SERIKALI
kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepanga kutekeleza Ajenda ya maendeleo
endelevu ambayo pamoja na Mambo mengine imeainisha malengo 17 ya Maendeleo
ambayo kwa kifupi yanajulikana Kama SDGs malengo hayo yanaonesha shabaha ambazo
Dunia inategemea kufikia ifikapo mwaka 2030
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 8 Jijini Dodoma
na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango
Jennifer Omolo kwenye hafla ya
uzinduazi wa Ajenda ya maendeleo endelevu yenye lengo na mkakati wa kukuza
Uchumi na Kupunguza Umasikini kwa upande wa Tanzania bara ambao ni maarufu Kama FYDP na ZADEP kwa upande wa Zanzibar
Amesema
kufuatia ujumuishaji huu mipango pamoja na bajeti zote za kisekta zimeendelea
kuasili na kutumika kama nyenzo kuu ya serikali ya utekelezaji wa afua za SDGs
ili kuongeza kasi utekelezaji wa SDG na kufuatilia malengo yote 17
Serikali kupitia ofisi ya takwimu iliainisha maendeleo ya kijamii tukizungumza swala la maji tunataka watu wajue serikali imepambana kwa kiasi gani kutoka miaka ya nyuma na sasa tukizungumza Afya tunamanisha taarifa za mapitio zinapaswa kusimamiwa na serikali pamoja na tasisi binafsi
Tanzania inapaswa kuwasilisha katika jukwaa kuu la kisiasa nchini Marekani V.N.R mchakato wa kufanya utafiti wa SDGs linajumuisha sekta zote pamoja na taasisi
Jennifer
Naye
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Elimu
Sayansi na Teknolojia Bw Frank Rozamula amesama kutokana na utekelezaji
wa malengo ya maendeleo endelevu Wizara ya Elimu inagusa kila mtu na
inazingatia ubora wa Elimu na inawafikia watanzania
Wizara ya elimu tumefanya mambo mengi kwanza tumejenga miundombinu kama madarasa kwa shule za msingi na shule za sekondari ili kuhakikisha watoto hawapati shida sehemu ya kujifunzia pamoja na vitabu lakini tumetoa mafunzo kwa walimu walio shuleni na walio mafunzoni tumetoa vishikwambi kwa walimu
Kwa upande wa elimu ya juu tumejenga kampasi 17 katika mikoa minne ili kufikia maeneo ambayo hayana vyuo vya Kati na kila mkoa tumepanga kujenga shule ya watoto wa kike na kila shule itakuwa wa wanafunzi 1000
Rozamula
0 Comments