SERIKALI KUANZA MCHAKATO WA KUPISHA MITAALA NGAZI ZA ELIMU YA JUU KUBAINI MAPUNGUFU

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

SERIKALI kwa kushirikiana na sekta binafsi NCHINI wameanza mchakato wa kupitia mitaala ngazi ya elimu ya juu ili kubaini mapungufu yaliyopo kwa wahitimu wa vyuo katika Soko la ajira huku sekta binafsi ikitakiwa kuainisha changamoto wanazozibaini kwa wahitimu wanaowajiri.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati Maalum inayojumuisha wadau wa elimu na waajiri kutoka sekta binafsi itakayokwenda kufanya tathmini ya mitaala, Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda amebainisha malengo ya kuunda kamati hiyo.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo kikuu Cha Dodoma (Udom) Profesa Lugano Kusiluka amesema wamelenga katika kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu 

Profesa Kusiluka  amesema wana dhamana ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa vizuri na kufanya mageuzi na maboresho makubwa kwenye taasisi za elimu ya juu na hasa vyuo vikuu vinavyotoa program zake na namna gani hizo program zitaleta tija kwa wahitimu wake na hata kule wanapokwenda kufanya kazi.

Tuna imani kwamba katika kipindi hiki kwa aina ya program zinazoenda kutolewa na aina ya wahitimu watakuwa tofauti na miaka ya nyuma

Kusiruka 

Naye Mratibu wa mradi wa  HEET UDOM,  Profesa Razaki Lokina amesema  kuna kipengele cha kusomesha wanataaluma katika ngazi mbalimbali ngazi za Masters na PHD ambao wanafunzi wapo mashuleni lakini pia kuna kipengele cha ujenzi miundombinu na kuimarisha mifumo ya mahusiano ya internet chuoni  kama chuo lengo lao  wamejipanga kuwa na HEET katika mitaala yote 

Aidha amesema lengo ni kuona mchakato huo kupitia mitaala ngazi za elimu ya juu ni  pamoja na kuwa na wahitimu wanaoajirika katika soko.

Lengo ni kuwa na wanafunzi wanaoingia kwenye soko la ajira na ambao wanahitajika badala ya kuwa na wanafunzi ambao tunaanza kuwafundisha tena ili hata mwaajiri aweze kunufaika

Profesa Razack



 

Post a Comment

0 Comments