SERIKALI IMESEMA UJENZI WA KITUO CHA POLISI KISHAPU UMESIMAMA UKIWA KWENYE HATUA YA UMALIZIAJI

 ðŸ“ŒSAIDA ISSA

SERIKALI imesema kuwa Kituo cha Polisi Wilaya ya Kishapu ni kituo cha daraja B, na ujenzi wake umesimama ukiwa umefikia kwenye hatua ya umaliziaji.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Jumanne Sagini alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo alipouliza Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa fedha ili kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya Kishapu?

Tathmini kwaajili ya kumalizia ujenzi imefanyika na kiasi cha fedha Tsh. 262,672,520/= zinahitajika,

Fedha hizo zimepangwa kutolewa kwenye mfuko wa tuzo na tozo kwa mwaka wa fedha 2023/2024,"alisema Naibu Sagini.

Aidha amesema kuwa Fedha zitakapotolewa ujenzi huo utakamilishwa ili wananchi wa Kishapu waanze kunufaika na huduma za polisi kupitia kituo hicho.

 

Post a Comment

0 Comments