RAIS WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA ATOA TAMKO

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

CHAMA Cha walimu Tanzania kinakemea vikali  kitendo cha Naibu Katibu Mkuu wa CWT Mwl. Joseph Misalaba, Kaimu Mweka Hazina wa CWT Taifa Mwl Protas Magesa na baadhi ya wajumbe ambao ni viongozi wakuu wa kitaifa pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati tendaji baada ya kupitisha kikao cha dharura na kusimamisha majukumu ya kazi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Mwl Maganga Japhet .

Akitoa tamko hilo Rais Chama cha walimu Tanzania Mwl Leah Ulaya amesema viongozi hao na wajumbe hao wamevunja katiba na kanuni za CWT kwa maslahi yao binafsi na kuchafua taswira na heshima ya CWT kwa wanachama .

Amesema kitendo cha Mwenyekiti na katibu wa Kamati tendaji Taifa kupitisha kikao na kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari ni batili na wamepoka Mamlaka na madaraka ya Rais wa CWT kinyume na Ibara ya 23 (23.1) (C) ya katiba ya CWT .

Ili kuondoa sintofamu iliyotokana na kikao batili  cha Kamati tendaji Taifa  cha Tarehe 6 Juni 23 pamoja na maazimio yake Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri  kupitia Kumbukumbu namba. DA 27/380/12/21 amethibitisha maazimio ya kikao hicho na utekekezaji wake hakikuwa halali na kilifanya maamuzi batili ambayo hayakuzingatia katiba na kanuni za CWT

Mwl Leah Rais wa CWT.

Amesema wadau mbalimbali wanawatambua kwa nafasi zao kama viongozi wa CWT na watumishi wa Umma wanapaswa kuwa mfano Bora wa kuigwa na jamii hivyo wanachama, wadau , watumishi wa CWT na Umma kwa ujumla wapuuzie maazimio ya kikao hicho haramu kilichofanywa kwa nia ovu.

Aidha amewataka wanachama, watumishi, viongozi wote wa CWT na wadau kuendelea kupokea taarifa za kiutendaji za Chama kutoka kwa Mwl Maganga Japhet ambaye ndio Katibu mkuu wa Chama cha walimu Tanzania aliyechaguliwa na mkutano mkuu halali wa CWT. 

Hata hivyo amewataka wanachama na wadau wote wanaombwa kuwa na subira wakati Chama kikiendelea kuchukua hatua stahili za kinidhamu kwa wote walioshiriki kuvunja katiba na kanuni za CWT kwa makusudi.

Wanachama wote wa CWT, viongozi na watumishi tuendelee kuwa na umoja na mshikamano kwani ndiyo nguvu ya wafanyakazi

 Mwl Leah

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments