MWONGOZO WA USIMAMIZI WA PAMOJA WA MIUNDOMBINU ILIYOKO CHINI YA ARDHI WAZINDULIWA.


 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

SERIKALI imezindua mwongozo wa usimamizi wa pamoja wa miundombinu iliyoko chini ya ardhi kwenye mikuza inayotumiwa na taasisi na kampuni za huduma mbalimbali lengo likiwa ni kuimarisha usalama wa umma, kuongeza uadilifu na usimamizi makini wa miundombinu iliyopo chini ya ardhi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Kamishna wa Petroli na Gesi Asilia  kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Michael Mjinja amesema kuwa mwongozo huo utasaidia katika kuimarisha usalama na kuwa na usimamizi makini kwenye miundombinu iliyopo chini ya ardhi. 

Amesema kuwa usimamizi wa pamoja wa Miundombinu iliyoko Chini ya Ardhi kwenye Mikuza (wayleave) wa Mwaka 2023, unazinduliwa kwa dhumuni la kuimarisha usalama wa umma, kuongeza uadilifu na usimamizi makini wa miundombinu iliyopo chini ya ardhi Tanzania Bara.

Mwongozo huu utasaidia katika kuratibu shughuli za ujenzi, uendeshaji, marekebisho na matumizi mengineyo ya mikuza inayotumiwa kwa pamoja na wadau mbalimbali bila kuathiri usalama wa miundombinu, umma na mali zao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dk. James Andilile amesema kuwa mamlaka hiyo imeratibu zoezi la uandaaji wa mwongozo huo kuanzia mwaka 2019 pamoja na timu za Wataalamu kutoka kwa wamiliki na watumiaji wa Mikuza na Wakuu wa Taasisi kwa kuridhia mwongozo huo.

Dkt. Andilile amesema kuwa miaka ya hivi karibuni usambazaji wa gesi asilia katika miji ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara umeongezeka. Ongezeko hilo limepelekea  shughuli za utandazaji wa miundombinu katika mikuza inayotumiwa na watoa huduma mbalimbali,  yakiwemo  mabomba ya usambazaji wa  mafuta na maji, miundombinu ya umeme na mawasiliano. 

Shughuli za uchimbaji ili kutandaza miundombinu kwenye mikuza  haziepukiki kwani mahitaji ya huduma zinazotolewa na kampuni mbalimbali zinazidi kuongezeka na kufanyika bila ya kuratibiwa; hivyo basi kusababisha uharibifu wa miundombinu iliyofukiwa chini ya ardhi, migogoro na  kuhatarisha usalama wa miundombinu hiyo, watu na mali zao.

Amesema kuwa kukosekana kuratibiwa kwa shughuli hizi, zinatokana na mikuza hiyo kumilikiwa na taasisi tofauti na zile zinazotoa huduma katika mikuza hiyo. Mikuza yenye muingiliano mkubwa wa miundombinuni.

Amesema kuwa baada ya maandalizi ya muda mrefu, timu ya wataalamu imekamilisha maandalizi ya mwongozo huo na rasimu ya mwongozo ilipitiwa na wamiliki na watumiaji wa mikuza.

Mwongozo huu utaratibu shughuli za ujenzi, uendeshaji, marekebisho na matumizi mengineyo ya mikuza 

Tunaamini wamiliki na watumiaji, wataufuata mwongozo huu katika utumiaji wa mikuza ili kulinda miundombinu hiyo, kuepusha migogoro na kuokoa maisha ya watu na mali zao

Naye mwenyekiti wa kamati ya  ya bodi ya nishati, Haruna Masebu  amesema kuwa kumekua na ongezeko la shughuli  zisizoratibiwa kwa pamoja katika utaratibu usio rasmi  kwenye miundombinu iliyoko chini ya ardhi.

Hali hii imepelekea athari kubwa za kiusalama, uharibifu wa mali, mazingira na ajali kwa watu, mfano ni ajali za kupasuliwa kwa mabomba ya gesi asilia, mafuta na maji wakati wa shughuli za ujenzi na maboresho ya miundombinu katika maeneo mbali mbali

Ameongeza kuwa juhudi hizo hazijafikia Taasisi na Kampuni zote zenye miundombinu chini ya ardhi kwa mfano mamlaka za maji mikoani, kampuni za mawasiliano na kampuni za madini.

Amesema kuwa makubaliano haya yalihusisha Taasisi na kampuni zifuatazo TAZARA, TAZAMA, SONGAS, TPDC, GASCO, TRC, TTCL, M&P LIMITED, TANROADS, PAET, TANESCO, DAWASA na TARURA. 



 

 

Post a Comment

0 Comments