MUSUKUMA AWATAKA WATANZANIA KUTOYUMBISHWA NA MANENO YA MITANDAONI

 ðŸ“ŒSAIDA ISSA

MBUNGE wa Geita vijijini Joseph Musukuma amewataka watanzania kutoyumbwisha na maneno ya watu wasioitakia mema Nchi bali waunge mkono judihada za Rais kwenye Uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam ambao utakuwa na tija kwa wafanyabiashara.

Mbunge huyo ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwepo kwa maneno kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisema bandari hiyo imeuzwa na wengine wakisema mkataba wa miaka 100.

Tuache kudanganyana mimi nimefika Dubai nimejionea namna bandari za wenzetu zinavyofanya kazi, Uwekezaji unaofanywa na Serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia utasaidia sisi wafanyabiashara kupunguza malalamiko ya kucheleweshewa mizigo bandarini

Musukuma.

Amesema kuwa hali iliyopo kwa sasa bandarini katika upokeaji wa mizigo unachukua muda mrefu na inapelekea wafanyabiashara wengi kuagiza mizigo kupitia bandari nyingine ikiwemo bandari ya Mombasa.

Taasisi ya Rais ina watu wengi sio kwamba wanavyozungumza mitandaoni hakuna tafiti zilizofanyika, Ikulu imefanya utafiti na sisi wabunge baadhi tulienda kuona na kuona ni kuamini, na sio wanaozungumza mitandaoni wanauwezo mkubwa sana sio kweli unaweza ukawa na uwezo mukubwa wa kuzungumza mitandaoni lakini hujui mateso yaliyopo bandarini ukabaki tu kushinda mitandaoni, kujadili wenzio na kupinga vitu ambavyo huna uhakika navyo

Musukuma.

Kadhalika aliwataka watanzania kuunga mkono azimio hilo na kama kuna mapungufu yatasimama kwenye mkataba kwani kwa sasa kinachojadiliwa ni makubaliano ya Nchi na Nchi.

Mimi naamini maneno yanayoandikwa kwenye Mitandao sio ya kweli kwasababu hata Rais Samia atastaafu na yeye ataishi maisha kama ya kwetu si kweli kama ataenda kusaini mkataba ambao hauna maslahi kwa Taifa hili labda yeye kama iwe akistaafu anahama Tanzania lakini hapana tusikatishane tamaa

Turudi nyuma watanzania hakuna mkataba wa kimkakati ambao tumeufanya kwenye awamu zote bila kuwa na kelele na kelele hizi zinatengenezwa na watu wasioitakia mema Nchi yetu,"alisema Msukuma.

 

Post a Comment

0 Comments