MRADI WA UJENZI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME IRINGA HADI SUMBAWANGA KUPITIA MBEYA NA TUNDUMA KUANZA JUNI 2023 NA KUKAMILIKA SEPTEMBA 2023.

 ðŸ“ŒSAIDA ISSA

SERIKALI imesema kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 620 kutoka Iringa hadi Sumbawanga kupitia Mbeya na Tunduma unatarajiwa kuanza mwezi Juni, 2023 na kukamilika mwezi Septemba, 2025. 

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza alipouliza Je, ni lini Ujenzi wa umeme wa kilovoti 400 kutoka Iringa – Mbeya – Tunduma –Sumbawanga utaanza pamoja na kuwalipa fidia wananchi waliopitiwa na laini hiyo.

Mradi huu unalenga kuunganisha Gridi ya Taifa na nchi za Kusini mwa Afrika (Southern African Power Pool – SAPP) na utagharimu jumla ya Shilingi trilioni 1.38

Naibu Waziri

Aidha amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari imetoa Shilingi bilioni 16.43 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi 6,500 wanaopisha mradi na kazi ya ulipaji fidia imekamilika kwa awamu ya kwanza ambapo wananchi 4,750 wamepokea Shilingi bilioni 13.67 na maandalizi ya awamu ya pili yanaendelea na malipo yanatarajiwa kufanyika ifikapo Julai 2023.

 

Post a Comment

0 Comments