📌WILSON JOHN
MAKAMU
wa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Philipo Isdor Mpango ametoa
maagizo matano kwa Baraza la taifa la kusimamia mazingira pamoja na mamlaka za
serikali za mitaa kote nchini kusimamia na kuongeza nguvu katika katazo la matumizi
ya mifuko ya plastiki kama vifaa vya kufungashia bidhaa
Kauli
hiyo ameitoa leo Juni 6 katika mkutano wake na wafanyabiashara wa soko la
Machinga Complex Jijini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho siku ya
mazingira Duniani iliyobebwa na kauli mbiu isemayo ' Pinga uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki'
Amesema
kumekua na ukiukwaji wa Sheria ambao unafanywa na baadhi ya wafanyabiashara
wanaoingiza kinyemela kutoka mataifa ya nje jambo ambalo linarudisha nyuma
maendeleo yaliyofikiwa na serikali
ilipotoa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki
Naziagiza Halimashauri zote nchini kusimamia Sheria ndogondogo walizozitunga kuhusu usafi wa mazingira na kuhakikisha mnawachukulia hatua wale wote watakao kiuka maagizo mliyo yaweka,
Lakini pia NEMC mzingatie kampuni zinazopewa majukumu ya kukusanya taka ziwe na utaratibu maalumu wa taka, kwahiyo ninazikumbusha Halimashauri kuacha kutoa tenda kwa kampuni zisizo na uwezo
Mpango
Hata
hivyo Makamu wa Rais amezitaka kampuni na wamiliki wa magari kuwa na sehemu ya
kuwekea taka katika gari ili kupunguza
usumbufu kwa abiria na utupaji wa taka ovyo pamoja na wazalishaji wa taka za plastiki kuhakikisha
taka zinazozalishwa zinakusanywa na kuondolewa.
Ni vizuri kila Kaya kuwa na sehemu ya kuhifadhi na kuchoma taka lakini pia wamiliki wa magari wekeni mazingira ya kuhifadhi taka ili kuepusha utupaji wa taka barabarani
Natoa wito kwa sekta binafsi kuongeza jitihada na juhudi ya kukusanya taka kwani taka zinaweza kuwa malighafi na kutumika kama bidhaa zingine, naiagiza Ofisi ya Mh, Suleiman Jafo mtafute wawekezaji kwa ajili ya hizi malighafi
Mpango
Kwa upande wake Waziri Ofisi ya Makamu wa
Raisi, Muungano na Mazingira Mh, Suleiman Said Jafo amesema Ofisi yake kwa
kushirikiana na Baraza la taifa la usimamizi wa mazingira (NEMC) wanahakikisha swala la usafi wa mazingira
linasimamiwa vizuri nchi nzima.
Mwaka huu tunataka kufanya tofauti kidogo twende kuleta shughuli za mazingira viwanjani zoezi hili lilianza katika uwanja wa shule ya Sekondari kiwanja cha ndege tulifanya kazi kubwa ya usafi wa mazingira
Na leo Mhe. Makamu wa Rais umefanya kazi kubwa ya kuwaongoza wafanyabiashara wa soko la Machinga Complex kufanya usafi hapa nataka nikuhakikishie kiongozi wa mbio za mwenge nchini Bw, Abdala Shaibu Kaim anasimamia kikamilifu suaala la usafi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki
Jafo
0 Comments