SERIKALI imesema
kuwa Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa Mikoa iliyofanya vizuri katika kuanzisha
majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ambapo, Jukwaa la Mkoa limeanzishwa
kwa mafanikio makubwa hadi kufikia wazo la kuanzisha kiwanda cha
vifungashio.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, wanawake na Makundi maalum Mwanaidi Ali khamis alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti maalumu Pwani Subiri Mgalu alipouliza
Je, Serikali ina mpango gani wa kuyapatia mafunzo majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi katika ngazi za Vitongoji, Vijiji, Kata na Wilaya Mkoani Pwani?
0 Comments