SERIKALI imesema kuwa Bodi ya Barabara ya
Mkoa wa Mbeya kupitia kikao chake cha tarehe 09 Januari, 2023, ilitoa
mapendekezo ya kuipandisha hadhi Barabara ya Mjele –Ikukwa hadi Mlima Njiwa
kuwa ya Mkoa.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa TAMISEMI Deogratus Ndejembi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza alipouliza Je, ni lini Serikali itaipandisha hadhi barabara ya Mjele – Ikukwa hadi Mlima Njiwa kuwa ya Mkoa?
Baada ya mapendekezo hayo kuwasilishwa kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, tarehe 24 Februari, 2023 Kamati ya Kitaifa ya Kupanga Barabara Katika Hadhi Stahiki (NRCC) ilitembelea barabara zilizoombwa kupandishwa hadhi Mkoani Mbeya ikiwemo barabara ya Mjele – Ikukwa hadi Mlima Njiwa,
Naibu.
Kadhalika amesema kuwa Mapendekezo ya Kamati yamewasilishwa kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na yanachambuliwa na uchambuzi ukikamilika taarifa itatolewa.
Endapo barabara hiyo itakidhi vigezo vya kupandishwa hadhi, itakuwa barabara ya mkoa na itahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD).
Mbunge Njeza amesema kuwa licha ya Waziri wa Ujenzi kuridhia barabara hiyo ihudumiwe na TANROAD ipo kwenye hali mbaya na ametaka kujua ni lini itaanza Ujenzi na iweze kurekebishwa kuanzia Mjele-ikukwa mpaka Mlima njiwa
Naibu Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema kuwa baadaya ya kupandishwa hadhi barabara hiyo TANROAD itaanza utejelezaji kwa bajeti ambayo itaanza mwaka wa fedha 2023/24.
Kwa sasa wenzetu wa TARURA baada ya Juni watatukabidhi na sisi tutaanza utekelezaji huo kwa bajeti mpya
Naibu wa Ujenzi na Uchukuzi.
Kadhalika Mbunge Njeza amesema katika hali hiyo ya barabara ipo barabara ya Aporoto-Ilea-Ishinda ambayo inahudumia wachimbaji wa migodi ya Ilea na Ishinda ni lini barabara hiyo itapata matengenezo sababu nayo ipo katika hali mbaya?
Naibu Waziri Ndejembi amesema kuwa barabara hiyo ilipokuwa TARURA ilitengewa Shilingi Milioni 500 na Roadboard kwaajili ya matengenezo yake.
Sasa baada ya kupandishwa hadhi fedha ile itahamia kwa wenzetu TANROAD ambapo bado watatelekeza kwenye barabara hii kwa hii shilingi Milioni 500 kwaajili ya kuijenga
Barabarani ya Aporoto-Ilea-Ishinda barabara hii ina urefu wa kilomita 9 na kweli nikiri kwamba barabara hii hali yake si nzuri sana katika mwaka wa fedha ambao tunauanza mwezi unaofuata huu tayari barabara hii imetengewa shilingi Milioni 400 kwaajili ya kuweza kutengeneza yale maeneo korofi kwa kumwaga changarawe na kuhakikisha kwamba inapitika vizuri sababu inapelekea katika eneo ambalo lina machimbo hivyo nimtoe hofu mbunge Njeza muda si mrefu ataona utekelezaji wake
Ndejembi.
0 Comments