MBUNGE NJEZA AIOMBA SERIKALI KUKAMILISHA KWA HARAKA UJENZI WA SGR NA RELI YA TAZARA

📌SAIDA ISSA

KUTOKANA na maboresho ya bandari yanayofanyika Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza ameiomba Serikali kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa SGR kwa muda mfupi pamoja na Ujenzi wa reli ya TAZARA kwani ni muhimu kwa biashara ya bandari sababu kutakuwa na ongezeko la mizigo.

Hayo ameyaeleza Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akichangia Hoja ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24 amesema kuwa baada ya kukamika kwa maboresho ya bandari ya Dar es salaam kutakuwa na ongezeko la mizigo.

Mizigo mingi itaongezeka na hiyo mizigo asilimia 70 ya mizigo yote haitakuwa bora ianze kupita tena kwenye express way tupitishe kwenye reli ambayo itafanya gharama za usafirishaji za kwetu ziwe za chini ukilinganisha na Nchi zingine

Kadhalika ameiomba Serikali kuhakikisha inaboresha biashara ya madini kwa sasa madini ndio yanayoleta pesa za kigeni katika nchi.

Pamoja na kupambana na hali ya Uchumi naiomba Serikali iangalie zaidi na iweke kipaumbele cha kwanza kuhakikisha inaboresha biashara ya madini.Madini ndio yanayotuletea pesa za kigeni sasa hivi

Mheshimiwa mwenyekiti nimeona Juzi na nampongeza tena Mheshimiwa Rais ameidhinisha kulipa fidia ya wananchi wa Liganga walipwe zaidi ya shilingi Bilioni 15 kwaajili ya kufua ule mradi mkubwa,"amesema Mbunge Njeza.

 

Post a Comment

0 Comments