MTEKINOLOGIA
wa chakula kutoka bodi ya maziwa Tanzania Neema Moshi amewashauri wagonjwa
kutumia maziwa salama yenye virutubisho kama chakula ili kuwasaidia kuimarisha
afya zao.
Ameyasema
hayo Leo Jijini Dodoma wakati Bodi ya Maziwa Tanzania ikiwa ni sehemu ya kuwatembelea
wagonjwa Hospitali ya Rufaa jijini Dodoma
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki
ya watumishi wa umma.
Amesema
pamoja na kutoa msaada wa maziwa kwa wagonjwa pia wametoa elimu kuhusu umuhimu
wa maziwa kwa ajili ya kulinda afya zao.
Maziwa sio dawa ya vidonda vya tumbo hapana ila wagonjwa wa vidonda vya tumbo wanashauriwa kutumia maziwa baada ya kula ambapo watatumia glass moja ya maziwa ili kupunguza maumivu na kupata nguvu pia maziwa yanatumika kama kiburudisho
Kwa wagonjwa wote tumieni maziwa ili kuongeza nguvu lakini kwa wale wanaotumia dawa kuna dawa unaweza kunywa huku ukitumia maziwa na kuna dawa huruhusiwi kutumia maziwa hivyo ni vizuri kuongea na daktari kama dawa hiyo inafaa kutumia na maziwa
Neema .
Kwa
upande wake Kaimu Muuguzi Mfawidhi hospitalini hapo Patricia Kabendela amesema
maziwa ni chakula kilichokamilika hivyo kinahitajika mwilini na kwenye damu pia.
Amewataka watu kutumia maziwa hayo kwakuwa yanaongeza nguvu mwilini na kusema
kuwa ni bora sana kwa watu wazima kuliko mtoto ambapo kwa mtoto maziwa ya mama
ndio bora zaidi
Hata
hivyo mama mzazi mwenye watoto wawili (2) wagonjwa
Jenipha Mwali ameishukuru bodi ya maziwa
kuwapatia wagonjwa maziwa hayo na kusema kuwa yatawasaidia kuboresha afya zao
ili zibaki imara, pia amewataka wagonjwa waliopatiwa maziwa kuyatumia ili
waboreshe afya zao.
Tunawashukuru bodi hii kutupatia maziwa ambayo yatatusaidia katika kuboresha afya zetu na muendelee kuwa na moyo wa kutoa, pia nawashauri wagonjwa kutumia maziwa waliotupatia ili kulinda afya zetu
Jenipher
0 Comments