LATRA HUPANGA RATIBA YA MABASI YOTE YA MASAFA MAREFU"NAIBU WAZIRI MWAKIBETE"

 ðŸ“ŒSAIDA ISSA

NAIBU Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Atupele Mwakibete amesema kuwa Mabasi yote ya masafa marefu hupangiwa ratiba na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ambazo huonyesha stendi za kupakia na kushusha abiria pamoja na muda wa kusimama kwenye stendi hizo.

Naibu Waziri Mwakibete ameyasema hayo Leo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Igunga Nicholas Ngassa alipouliza Je, Serikali inatoa tamko gani kwa mabasi yasiyoingia stendi na ambayo hushusha abiria nje ya Stendi?

Mheshimiwa Spika, Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Igunga kama ifuatavyo:- mabasi ya masafa marefu yamepangiwa kusimama katika Stendi moja tu kwa kila Mkoa isipokuwa pale ambapo basi hilo lina abiria anayeshuka katika Stendi ya Wilaya

Naibu Mwakibete. 

Kadhalika amesema kuwa Utaratibu huo umepangwa ili kuondoa usumbufu na ucheleweshaji wa abiria wa masafa marefu kwa kuwalazimisha kuingia kwenye Stendi hata kama hawana abiria wa kupanda au kushuka. 

Kwa kuwa Mhe Ngassa anatoka Igunga, naomba kumtaarifu kuwa, stendi ya Igunga haimo kwenye Stendi ambazo mabasi ya masafa marefu hulazimika kuingia au kusimama isipokuwa kama yana abiria wa kupanda au kushuka kwenye Stendi hiyo Amesema kuwa Stendi hiyo hutumika kwa magari yote yanayotoa huduma ndani ya mkoa wa Tabora na mikoa jirani.

Ameeleza kuwa kwa madereva wanaokaidi kuingia Stendi na kushushia abiria nje ya Stendi hususan barabarani, madereva hao wanakiuka maelekezo ya kifungu cha 50(1) cha Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 kinachomzuia mtu yeyote kuegesha au kusimamisha gari barabarani bila kujali watumiaji wengine wa barabara, hivyo, wanavunja Sheria.

 

Post a Comment

0 Comments