SERIKALI imesema
kuwa kwa kuzingatia vihatarishi vilivyopo kwenye miamala husika, imekua
ikichukua hatua mbalimbali zinazolenga kuimarisha udhibiti na kuzuia upotevu wa
mapato.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Chande alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa alipouliza Je, ni kwa kiwango gani Serikali imejiimarisha kukagua miamala ya uhamishaji wa bei ya mauziano ya bidhaa na huduma baina ya Makampuni ya Kimataifa?
Mheshimiwa Spika, Kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mpina Serikali imeimarisha mifumo ambayo itadhibiti mianya yote na rushwa na njia nyingine za ukwepaji wa kodi
Pamoja na hayo Serikali kupitia TRA imeongeza rasilimali watu kwa kiasi kikubwa sana na hata hivi karibuni nafasi 524 zimetangazwa na mchakato unaendelea
Chande.
Kadhalika amesema kuwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuanzisha a)Kitengo Maalum cha Usimamizi wa Kodi za Kimataifa ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kuanzia 2011;
b) Kuandaa na
kusimamia utekelezaji wa kanuni na miongozo kuhusu Ukaguzi wa kodi kwenye
kampuni zenye mahusiano,
c)TRA imenunua Kanzidata ya Orbis kwa ajili ya kupata taarifa za kusaidia kufananisha bei za Miamala ya Kimataifa ili zisaidie kujenga hoja wakati wa ukaguzi unaofanywa kwenye Kampuni za hapa nchini; na d) Tanzania imejiunga na Jukwaa la Kimataifa la Ubadilishaji wa Taarifa za Kikodi kwa lengo la kuhakikisha nchi yetu inajenga uwezo wa kubadilishana taarifa za kikodi na nchi nyingine.
Pia amesema kuwa Serikali inatarajia kusaini Mkataba ujulikanao kama “Multilateral Convention on Mutual Administrative Assistance in Tax Matters” ambao utaiwezesha TRA kupata taarifa mbalimbali kutoka katika nchi 146 duniani ambazo zitasaidia katika kuongeza ufanisi wa ukaguzi wa Miamala ya Kimataifa.
0 Comments