SERIKALI
kupitia Wizara ya Maendeleo ya jamii wanawake na makundi maalum imetakiwa kutoa elimu itakayosaidia wanawake
kuchangamkia fursa za biashara na manunuzi ikiwemo kuwapatia mikopo na riba
nafuu ili kuwawezesha wanawake
kujikwamua kiuchumi
Kauli
hiyo imekuja mara baada ya ripoti ya tafiti za Afrika Mashariki kuhusu Pato la
taifa (yaani Gross Domestic Product GDP) yenye kujumuisha thamani ya Pato la
mwisho litokanalo na bidhaa fulani katika mwaka ambapo kwa Afrika Mashariki,
Kenya inaongoza kuliko Tanzania, Uganda na Rwanda
Ripoti
hiyo imesomwa na Gilbert Sendigwa Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika Freedom of
Information (AFIC) ambapo amesema wanawake wapewe elimu ili waweze kuchangamkia
fursa za biashara na manunuzi iliwaweze
kujikwamua kiuchumi maana tafiti zinalenga kuwanufaisha wanawake vijana na
makundi maalumu
Amesema
serikali kwa kushirikiana na taasisi pamoja na wadau mbalimbali waweze kutoa
elimu hususani kwa watu wanaoishi vijijini ili waweze kunufaika na fursa za
manunuzi kwa sababu watu wanaoishi vijijini wanachangamoto kubwa na uelewa
mdogo kuhusu fursa za manunuzi ya bidhaa pamoja na fursa zinazotolewa na
serikali
Mamilioni ya wanawake hawajui kuhusu fursa za manunuzi kwa sababu hawana taarifa ya kutosha kuhusu fursa hizo lakini pia changamoto nyingine ni mitaji serikali ikiwawezesha tutaondokana na changamoto hii,
Tunafanya mipango mingine kuhusu uchumi kusambaza wataalamu ili waweze kuhamasisha wanawake kuhusu fursa za manunuzi na biashara ili waweze kuzalisha vitu Bora
Sendigwa
Naye
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Dodoma Mh, Fatuma Tofiki amesema serikali
imetunga Sheria ambayo inalenga kutenga asilimia kumi 10% kwaajili ya wanawake
vijana na makundi maalumu ambapo amesema inatumia mfumo wa 4,4,2 ikiwa na maana
ya asilimia 4% zinatengwa kwaajili ya
wanawake asilimia 4% kwa vijana pamoja na asilimia mbili 2% kwa ajili ya makundi maalumu
Utafiti unatupa picha halisi ya manunuzi kwa wanawake pamoja na kuwa na Sheria hii lakini wanawake wananufaika vipi, kutokana na taarifa wenzetu wamepiga hatua kuliko sisi, Sasa tunataka tuone ni jinsi gani tunaweza kuwabeba wanawake
Takwimu
zinaonesha kuwa nchi ya Kenya imepiga
hatua ukilinganisha na nchi zingine katika kukutana na wanawake pamoja na
kuzungumza nao ili kuweza kuwapatia elimu itakayowawezesha na kunufaika na fursa
za manunuzi na biashara kwa wanawake ambapo takwimu zinaonesha asilimia 36%
ikifuatiwa na Ethiopia 30% Uganda 23% huku Tanzania ikiwa na asilimia 20% na
ikifuatiwa na Rwanda 15%
0 Comments