ONGEZEKO
la Ajira za utotoni limepelekea watoto wengi kuacha Shule na kukimbilia
mtaani wakitembeza matunda, mayai, na
vyakula mbalimbali huku wengine wakifanya vibarua vya kuchunga mifugo kwa ajiri
ya kujipatia riziki ili waweze kukidhi mahitaji yao na familia zao kiujumla, huku
wazazi wakiwa ndio chanzo cha kuwatafutia vibarua watoto wao
Hali
hii imeshamiri sana kwa maeneo ya mjini na vijijni kwa kiasi. Watu wengi wamekuwa
wakiamini kuwa watoto wakipata kazi au wakifanya vibarua ni njia mojawapo ya
kujikwamua kimaisha kitu ambacho kinapelekea ongezeko la umasikini kwa familia
na watotot kupoteza haki zao za msingi kama kupata elimu
Hali
hii inapelekea ongezeko la vikundi vya kiharifu na vibaka mtaani kutokana na
vijana wengi kukosa kazi na kuzunguka mtaani kitu ambacho huwafanya wakutane na
makundi yasiyofaa na tabia mbaya za uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya kwasababu
hawana mtu wa kuwasimamia.
Kauli
hiyo imetolewa na balozi wa Mtaa wa Salama kata ya Nkuhungu jijini Dodoma Bi.
Iricy Mbogoni amesema wazazi wenyewe
hawana mwamko wa kuwapeleka watoto shule
kutokana na ugumu wa maisha kitu ambacho hupelekea kuwashawishi watoto waache
shule
Amesema
ni kawaida sana watoto kwa upande wa mjini kuacha shule tofauti na vijijini
kwani serikali za mtaa kwa upande wa vijijini wanasimamia sana na wazazi wana ile
hali ya uoga wa kuhofia serikali tofauti na mjini
Hali hii inachangiwa na wazazi wenyewe kwa mfano kijana wangu alinipa taarifa kuhusu kijana mwenzake ambaye aliamua kuacha shule na wazazi wake walipofika shule wakaripoti mtoto hataki kusoma hivyo akapewa barua ya kuacha shule
Niiombe serikali na wadau wa elimu kutoa semina itakayo saidia watoto kupenda shule kama kijijini watu wanahofia serikali kuwa usipompeleka mtoto shule utachukuliwa hatua ningependa na sheria hii izingariwe kwa upande wa mjini
Iricy
Peter
Musa ni kijana wa pili kati ya watoto wanne katika familia ya mzee Musa Wilayani Bahi jijini dodoma amesema wazazi wake walimtafutia
kibarua cha kuchunga ng'ombe katika kata ya chang'ombe 'A' jijini hapo kwa ajili
ya kujipatia riziki
Amesema
kaka yake mkubwa naye yupo Kigoma kwa shughuli za kuchunga ng'ombe na kila mwisho wa mwezi wanatuma pesa
nyumbani ili kuwasaidia wazazi kulea
familia yao pamoja na kuwatunza wadogo zao
Shule niliishia darasa la pili baada ya hapo sikuweza kuendelea tena hii ilisababishwa na wazazi kushindwa kuninunulia mahitaji ya shuleni na nilipofikisha miaka kumi 10 wazazi walinitafutia kibarua cha kuchunga ng'ombe mpaka sasa nafanya kazi hiyo.
Kila siku asubuhi nawakatia nyasi na jioni saa kumi nawatoa kwa ajili ya kuwapeleka malishoni na kila mwisho wa mwezi napewa laki moja na elfu hamsini(150,000/=)
Peter
Kwa
upande wake Abdalah Hussein amesema yeye aliacha shule sababu ya
mila yaani jando alipofika darasa la sita wazazi walimpeleka jandoni
hivyo alichelewa kufanya mtihani, alip rudi shule walimu wakamrudisha darasa akaamua
kuacha shule
Amesema
kwa sasa anajishughulisha na biashara ya bajia akizungusha katika Soko la
Machinga Complex kazi ambayo huifanya kwanzia saa 12 alfajiri hadi jioni na
pesa akipata anapeleka kwa mwajiri wake
Kwa siku naweza nikauza hadi elfu sitini (60,000/=) na pesa inayopatikana nampelekea mwajiri wangu ambapo yeye hunilipa elfu tatu (3,000/=) kwa siku pesa hii ninayopata napeleka nyumbani na kuweka kwenye kibubu changu mwenyewe.
Walimu walipotaka kunirudisha darasa la sita niliwaeleza wazazi na wao wakaniruhusu kuacha shule baadaye wakanitafutia kazi ya kuuza bajia nafurahia kazi hii kutokana na pesa ninayopata kwani ni bora kuliko kubaki shuleni nirudie darasa
Hussein
Hata
hivyo watoto wa kike nao ni wahanga wakubwa wa ajira za utoto kwani huzunguka
mitaani wakiuza matunda na karanga kwenye masinia biashara ambazo wamepewa
mitaji na wazazi wao
Naomi
Mathias yeye ni binti mwenye umri wa miaka kumi na nne (14) amesema anawasaidia
wazazi wake kuuza karanga na matunda
katika eneo la Area C jijini Dodoma mara moja moja wakati baba yake akiwa na
majukumu mengine
Amesema
mama yake ni mama lishe hivyo baba akiwa na majukumu mengine yeye hubeba jukumu
la kuuza karanga na matunda lakini kama baba hana kazi hukaa na mama yake
gengeni akimsaidia kazi ndogo ndogo
Nimesoma hadi darasa la sita baadaye baba akasema nimsaidie mama kazi ndogo ndogo gengeni na baadaye niliacha kabisa kwenda shule kutokana na kazi ninazofanya
Sipendi kukaa hapa mimi nilipenda sana kusoma lakini wazazi wangu hawataki nisome na Mimi siwezi kuwapinga wazazi wangu
Naomi
Kifungu cha 4 cha Sheria
ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka, 2004 kinamuelezea mtoto kama mtu mwenye
umri chini ya miaka 14 isipokuwa kwa ajira zilizo katika sekta hatarishi, mtoto
maana yake ni mtu mwenye umri chini ya miaka 18
Hata
hivyo sheria inakataza mtoto mwenye umri chini ya miaka 14 kuajiriwa. Sheria pia
inaendelea kukataza ajira kwa watoto chini ya miaka 18 katika maeneo ya migodi,
viwanda, na mabaharia katika meli au kazi nyingine yeyote inayotambulika kuwa hatarishi.
Hata
hivyo,sheria inaruhusu ajira kwa watoto wa miaka 14 katika kazi nyepesi ambazo sio
hatarishi kwa afya ya watoto na maendeleo na haihatarishi mahudhurio ya watoto
shuleni, mafunzoni au program za kujifunza, Kwa ujumla ustawi wa watoto hautakiwi
kuhatarishwa hata kidogo
0 Comments