Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma akisisitiza jambo wakati wa Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya Habari jana (21/05/2023) yaliyofanyika kimkoa katika Ukumbi wa Roma Complex |
📌WILSON JOHN & AMISA AMIRI.
MWENYEKITI wa Klabu ya Wandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma Bw. Musa
Yusufu amewataka Wandishi wa habari jijini hapo, kujithamini
na kujitambua katika taaluma ya Uandishi
na Utangazaji lakini pia kupendana na
kupatana wanapotofautiana miongoni mwao na sio kutupiana vijembe wala kujenga
chuki baina yao.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa Maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari Duniani ambayo Kimkoa (Dodoma ) yamefanyika
tarehe 21 Mei, 2023 katika Ukumbi wa Roma complex ambapo wanahabari wanachama
wa Klabu walifanya Mdahalo katika kuchagiza kauli mbiu ya mwaka 2023 ambayo
inasema “Kuunda mustakabali wa Haki, Uhuru
wa kujieleza kama kichocheo cha Haki nyingine za binadamu”
Bw.
Musa Yusufu amesema tabia ya kununiana na kuchukiana inajenga taswira mbaya
katika jamii kwa Wandishi wa habari na kushusha thamani ya Wandishi wa habari
Wandishi tupendane na kuheshimiana miongoni mwetu, maana kuna watu wananuniana na kutupiana vijembe, sasa haya mambo yaishe leo tuzungumze pamoja na kushirikiana katika kazi
Niwaombe ndugu wandishi kila mmoja afanye kazi yake, kuna tabia imejitokeza sio nzuri na inatushushia heshima. Suaala la kwenda kwenye mkutano hujaalikwa baadae unataka usaini ili upate pesa si jambo zuri. Kama hujaalikwa nenda kachukue habari kisha waachie wahusika mambo mengine
Yusufu
Kwa upande wake mjumbe na mwaandishi wa habari
Mkongwe Joyce Kasiki amesema nidhamu kwa
wandishi wa habari imeshuka kadri siku zinavyozidi kwenda. Amesema baadhi ya
wandishi wa habari wamekua na tabia mbaya kiasi cha kushusha heshima kwa tasnia
ya Uandishi wa habari kutokana na tabia zisizofaa miongoni mwao.
Niwazungumzie Wandishi wapya, wakati sisi tunaanza kazi suala la kuhudhuria mikutano na kupata fedha tulikua tunalisikia kwa mabosi wetu lakini sasa mtu anaanza kazi leo kesho kuna mkutano Morena na pesa anachukua, sasa mtu huyu hawezi kufanya kazi kwa weledi
Nasikitika kusikia kuwa kuna watu wana zaidi ya vyombo vinne hadi vitano linapofika suala la kusaini mtu anajitokeza na kasema fulani kasema nimchukulie hii, inashusha thamani kwa Wandishi wa Habari tubadilike
Joyce
Kuna wandishi jinsi wanavyovaa na mwandishi huyo huyo anahitaji kupata story jambo ambalo watu wamekua wakitushangaa na kutuzungumzia hawa ni wandishi? Kwa jinsi tunavyovaa
Kwa
upande wa maslahi Okuly amesema
Imefikia wakati watu Sasa tunatishiana kisa mtu hajapata fedha, kwenye mkutano hujaalikwa halafu unataka usaini, mtu huyuhuyu ukionesha kumkatalia anaanza kukutishia hebu tuache hayo mambo tufanye kazi
Okuly
Makamu
Mwenyekiti wa Klabu ya Wandishi wa habari Karate Mbashiru amewataka Wandishi wa
habari kuheshimiana na kujitambua na kusema ukiwa mwaandishi moja punguza
ujuaji, kubali kujifunza na kukosolewa.
Maadhiisho
ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 3 Mei.
0 Comments