WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dk.Dorothy Gwajima amewataka wazazi na walezi kusimamia malezi ya watoto wao kikamilifu ili kulinda Maadili kwa watoto na Jamii nzima.
Dk.
Gwajima amesema hayo Mei, 15,2023,jijini Dodoma katika maadhimisho ya kitaifa
ya familia yaliyofanyika katika viwanja
vya Nyerere square, na kusema kuwa suala la Maadili katika Jamii ya sasa yamekuwa tofauti na zamani ambapo wazazi walikuwa wakiwakusanya watoto wao na kuwaelekeza namna bora ya kuishi na Jamii
inayowazunguka.
Amesema
kuwa Maadili yanayohitajika katika Jamii ni Maadili yanayoanzia katika familia
kwa kuhakikisha kila mzazi anamrithisha mtoto Maadili bora ili kujenga taifa
bora la leo na kesho. Pia amesema kupiga na kuuwa kwa mzazi sio suruhisho tosha la mgogoro kwa
watoto hivyo ni bora kila mzazi
kuhakikisha anapata muda wa kukaa na kuangalia Maadili ya watoto wake ndani ya
familia kwa kufanya mazungumzo na kutatua changamoto zinazo wakabili watoto.
Tulinde sana watoto kuliko kitu chochote ili tuimarishe familia bora katika ustawi mzuri wa familia na taifa kwa ujumla na kupigania Maadili ya Jamii mzima. Maadili yakiwa mazuri hatutakuwa na tatizo lolote na hatutakuwa na mabadiliko ya kijamii kuhusu vitendo vinavyotokea hapa matukio haya ni kukosekana kwa Maadili ndani ya Jamii yetu.
Maadili sio kitu kidogo kwa watoto, wazazi tuwape maadili, malezi na mafunzo bora watoto itakuwa ni bora sana kwao kuliko kumpa zawadi. Ukimpa mtoto Malezi Bora yatamsaidia sana kuliko vitu vimpatia upendo wa siku moja, kwahiyo inabidi tuangalie sisi kama wazazi na walezi ni kitu gani watoto wetu wanastahiki ndani ya Jamii yetu..
Dk.Gwajima
Amesema
kutokana na kuwa na watoto wengi wa mitaani
inaonyesha kuwa wazazi hawapo makini kuwalea watoto wao kikamilifu kama
inavyopaswa na sababu kubwa ambayo walikuwa wakiitaja watoto hao wanaoishi
mitaani ni wazazi kutokutimiza majukumu yao .
Sasa basi tuwe makini kulinda na kuwapa Maadili wa watoto, viongozi, wazazi lakini pia machifu tusaidizane katika suala la Maadili huko kwenye maeneo yetu tutakuwa na watoto wema
Sisi kama wazazi lazima tuwe tayari kuhakikisha tunalinda watoto wetu na kutowanyanyapaa ili tu tuepukane na matendo tunayoyasikia niombe tu viongozi wa dini, machifu ili tuangamize haya mambo mengine tunayoyasikia ndani ya Jamii yetu
Naye
aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, amewahimiza
viongozi wa dini kutoa elimu ya dini katika kujenga Maadili katika Jamii jambo
ambalo litawasaidia watoto kuwa na makuzi na Maadili ya Mungu katika maisha
yao.
Viongozi wa dini tunawaomba muwe kipaumbele na tunawategemea sana katika suala la kuwapatia elimu ya dini ikiwemo na Maadili huko kwenye maeneo yenu nadhani nyie mtatusaidia katika hilo.
Elimu tunayoitaka kwa watoto wetu tukiipata basi Jamii tutakuwa tumeipeleka sehemu stahiki pia wewe kama mzazi kamili ni lazima kuhakikisha familia hasa watoto kujua Maadili yao ndani ya familia .
Kabudi
Pia
Dk.Gwajima amesema Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu
Hassan amejitoa kwa kujenga madarasa ili kukabiliana na ongezeko watoto wa
mitaani.
0 Comments