WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wametakiwa kuacha na vitendo vya Rushwa ya ngono na kutaka kufaulishwa Katika masomo yao na badala yake wahakikishe wanakuwa mstari wa mbele kupinga na kuzuia vitendo vya Rushwa ya ngono.
Hayo yamesemwa na rais wa Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati Prof. Said Vuai wakati akifungua Warsha ya utoaji wa Elimu juu ya kupinga vitendo vya Rushwa ya ngono pamoja na Elimu ya jinsia.
Warsha hiyo imewajumuisha wanafunzi pamoja na wahadhiri wa Chuo hicho iliyofanyika Jijini Dodoma
Rais huyo amewataka walimu waachane na vitendo vya Rushwa kwa kuwarubuni wanafunzi kwa kuwapa msaada wa kuwafaulisha mitihani yao.
Hakuna maendeleo yoyote bila ya haki na haki haiwezi kupatikana kama kuna Rushwa hivyo kama kijana umefaulu kwa njia ya Rushwa basi hata katika maeneo ya kazi utakayoenda yatakuwa na changamoto na kusababisha Rushwa
Rais .
Kwa upande wake mtoa mada kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Faustine Malecha amesema kuwa zipo tabia ambazo zinapelekea Rushwa ambapo ameitaja mojawapo ni pamoja na kuiga vitu ambavyo sio desturi ya watu wa Kitanzania vinapelekea vijana hawa kujikita katika Rushwa .
Zipo aina nyingi za rushwa ila Rushwa ya ngono katika Elimu ya juu imekithiri hivyo niwatake vijana acheni kutumia Rushwa ya ngono kwa kuhisi mtafanikisha maisha kwa haraka
Malecha
Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kina mama na uzazi Dk Gabriel Kitunusa amesema kuwa wanafunzi wengi wanapata Elimu zisizo rasmi huko mitaani kuhusiana na mambo ya jinsia na mambo ya uzazi na kupelekea kupata changamoto za kutoa mimba na kusababisha vifo.Pia amesema changamoto kubwa ambazo wanafunzi hawa wanakutana nazo ni kupata mimba zisizotarajiwa na wengine kupata maambukizi ya VVU pamoja na Magonjwa ya zinaa ambapo amewataka waachane na Elimu ya mitaani na mienendo mibovu ya kimaadili.
Ikumbukwe kuwa Ndaki ya Sayansi Asilia ya Hisabati ina jukumu la kufundisha, kufanya utafiti kutoa huduma kwa jamii kupitia utaalamu wa utafiti pamoja na malengo mengine yanayohusiana na Rushwa na maswala ya Afya ya Uzazi.
0 Comments