WAKAZI
wa Jiji la Dodoma wameiomba Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
kukamilisha mapitio ya Sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 ikiwemo
mitaala ya elimu na kuanza utekelezaji.
Wakitoa
maoni yao jana Jijini hapa mara baada ya bajeti ya Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia kuwasilishwa bungeni na Waziri wa Wizara hiyo, Prof Adolf
Mkenda wananchi hao wamesema mapitio ya sera hiyo yatasaidia watoto
kuongezeka shuleni na kutatua changamoto ambazo zinawakabili wanafunzi kielimu.
Mwalimu
wa shule ya Sekondari Meriwa, Shukrani Nollo, amesema kutokana na serikali
kuonekana ipo makini na Sera hiyo ya elimu imepelekea wao kama walimu kuheshimu
nidhamu ya shule ambapo zamani walimu walikuwa wakitoka muda wowote
wanapojisikia kuondoka bila kutimiza majukumu wanayo takiwa ambapo imekuwa
tofauti na sasa
Uboreshaji wa elimu kwa sasa kuna mabadiliko makubwa, kwanza elimu bure vijana wengi wamehamasika kusoma hata wazazi kwenye vikao wamekua wakijitokeza kwa wingi kutokana na kufatilia watoto wao
Kuboresha vifaa kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo zaidi hii itasaidia wanapo hitimu masomo yao waweze kujiajiri kiurahisi pia kuongezeka kwa mshahara, tumeona Mei mosi sisi walimu serikali imetufikiria katika kuongeza mshahara hii inahamasisha ufundishaji
Nollo
Kwa
upande wake Mwanafunzi wa Chuo Cha biashara (CBE) kampasi ya Dodoma Stera
Benedict amesema uboreshaji wa elimu unaoendelea utawasaidia katika
kuwatatulia changamoto ambazo wanakumbana nazo ikiwemo kupewa mikopo kwa ajili
ya kujilipia ada na kutengeneza miundombinu ambayo bado inaitaji
marekebisho chuoni hapo
Amesema
kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kuweza kusaidia na kuboresha mazingira ya
kujifunzia ikiwemo kufundishwa kwa vitendo ili kusaidia kupata uelewa mpana
Nashukuru kwa fursa ya mikopo kwani itasaidia sana kuweza kutatua changamoto za ada lakini pia kutupatia elimu itakayotuwezesha kupata ajira kwani hatuwezi kujiajiri wenyewe
Kuboresha miundombinu katika vyuo itasaidia kupunguza usumbufu, utakuta wanafunzi wengine wapo darasani halafu wengine wanahitaji darasa hii inapelekea changamoto" Benedictor amesema
Katika
mwaka wa Fedha 2023/2024 Waziri wa Elimu Adolf Mkenda amesema Wizara
itakarabati maktaba na miundombinu mashuleni pamoja na majengo ili kuweka
mazingira mazuri ya kujifunza kwa wanafunzi.
0 Comments