ILI kuepuka kutapeliwa katika usafirishaji wa vifurushi, vipeto na kupoteza bidhaa pindi zinaposafirishwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaasa wananchi kutumia watoa huduma waliosajiliwa na mamlaka hiyo.
Aidha kuhusu kutuma vitu ambavyo ni hatarishi TCRA imesema imekuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha mzigo unaosafirishwa hauna athari kwa wengine huku ikisema imefanikiwa kudhibiti utapeli mtandaoni kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kutoa huduma kwa kufuata miongozo katika kusajili na kuhakiki laini za simu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 18 bungeni jijini Dodoma katika maonesho ya banda la Mamlaka hiyo yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Lucy Mbogoro Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na mahusiano kwa umma TCRA amesema, tangu kukamilika kwa zoezi la uhakiki na usajili laini za simu tarehe 13.4.2023 amesema zoezi hilo limefanikiwa kudhibiti wizi na wale wote wanaofanya uharibifu mtandaoni watakamatwa.
Teknolojia inakuwa na kuna vijana ambao ndio kwanza wametoka miaka 17 wameingia miaka 18 kwahiyo nao wanahitaji matumizi ya simu sasa katika hawa vijana kuna wengine ni wema pia kuna wengine ni waharifu ambao wanaweza kufanya vitendo vya uharifu
Awamu hii ya sita chini ya Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tumeweza kithibitisha hilo kwa kufuatilia namba za idadi ya watu ambao wamekuwa wakiongezeka na kuzifungia baadhi ya laini ambazo zimekuwa zikitumika kwaajili ya kutapeli watu
Lucy
0 Comments