TAKUKURU NA DCEA KUUNGANISHA NGUVU VITA DHIDI YA RUSHWA NA BIASHARA DAWA ZA KULEVYA

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya (DCEA) zimesaini mkataba wa makubaliano ya kikazi yenye lengo la kuongeza ushirikiano na kupanua wigo katika kukabiliana na rushwa pamoja na biashara ya dawa za kulevya na matumizi ya dawa hizo nchini.

Akizungumza leo Mei 26 jijini Dodoma mara baada ya kusaini mkataba huo Mkurugenzi Mkuu Wa TAKUKURU CP Salum Hamduni amesema Rushwa imekuwa ni moja ya kichocheo kikubwa cha kushamiri kwa biashara ya dawa za kulevya hapa nchini.

Mara nyingi wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za kulevya hutumia rushwa kuwanyamazisha watendaji wasiokuwa waaminifu na waadilifu wa Mamlaka ya usimamizi wa sheria ili kufumbia macho vitendo haramu vya biashara ya Madawa ya kulevya 

Amesema kuna mahusiano makubwa kati ya Rushwa na Madawa ya kulevya ni kama pande mbili za sarafu moja.

Amesema katika makubaliano hayo ya Taasisi hizo mbili yanakwenda kutoa mafunzo kwa watumishi wa Taasisi hizo kwa kubadilishana taarifa muhimu, pamoja na kutoa elimu kwa umma kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo klabu za wapinga rushwa shuleni.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya Aretas Lyimo amesema tatizo la rushwa na madawa ya kulevya yana uhusiano na yote yapo katika ngazi ya kimaitaifa.

Rushwa na dawa za kulevya zinashughulikiwa na Shirika moja la umoja na mataifa, na kutokana na mfanano huo uunganishwaji wa juhudi hizi ni muhimu kwakuwa kutaenda kusaidia kutatua matatizo mawili kwa wakati mmoja

 Lyimo 

 

Post a Comment

0 Comments