📌MWANDISHI WETU
MKUU wa Mkoa wa
Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo Mei 29, 2023 ameendelea na ziara ya kikazi
ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni katika Shule ya wasichana Bunge,
ujenzi wa Shule mpya ya msingi katika eneo la Swaswa na madarasa ya awali
katika Shule ya msingi Kisasa ambapo ujenzi wake uko katika hatua za ukamilishaji.
Katika kaguzi hizo
Mhe. Senyamule ametoa maagizo kwa wasimamizi wa mradi kuhakikisha kazi
inakamilika kwa muda uliopangwa na kuzingatia viwango vya ubora huku akitoa rai
kwa wasimamizi wa ujenzi kukaa na mafundi ili kufanikisha ukamilishaji wake.
Mkoa wa Dodoma tumejipanga kukamilisha hizi kazi kwa wakati hivyo wataalamu mkae na mafundi mpitie kwa pamoja mpango kazi wa miradi hii ili tujue kila siku ni kazi gani inatakiwa kukamilika kwa siku husika ili itakapofika tarehe 15 Juni 2023 ujenzi uwe umekamilika
Senyamule
Aidha, Senyamule
amesema kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ametoa fedha zote kwa wakati hivyo hakuna sababu za kuchelewa kufanya manunuzi.
Amesema ni wajibu wa wataalamu kuhakikisha ununuzi wa vifaa vyote vinavyohitajika
vinapatikana ili mradi uweze kukamilika kwa muda uliopangwa.
Mkoa wa Dodoma kupitia mradi wa Boost umepokea kiasi cha
Shilingi Bilioni 10.6 kwa ajili ujenzi wa Shule mpya 16, vyumba vya madasa ya
msingi 163, madarasa ya awali 16, ujenzi wa vyoo 106, nyumba za walimu 03 na
darasa 01 la elimu maalumu.
Shule ya Msingi Kisasa imepokea kiasi cha Shilingi
Milioni 63.6 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 2 na vyoo 6 huku Shule ya Swaswa imepokea
kiasi cha Shilingi Milioni 318.8 kwa ajili ya kujenga Shule mpya itakayokuwa na
madarasa ya msingi 7, madarasa ya awali 2 na Vyoo 12.
0 Comments