NAIBU
Waziri wa kilimo Mhe.Antony Mavunde amewatoa hofu wajasiriamali jijini Dodoma
ikiwemo kuwawezesha kiuchumi pamoja na kuanzisha Tuzo ya MAVUNDE yenye lengo la
kuwapatia milioni ishirini kwaajili ya kununua mashine itakayosaidia kuongeza
uchakataji katika viwanda
Ameyasema
hayo leo Mei 30, Jijini Dodoma wakati akifunga Mafunzo ya zunguka na mama
program yenye lengo la kuinua uchumi wa wafanyabiashara wadogowadogo na uchumi
wa viwanda (WAUVI)
Mh.
Mavunde amesema wajasiriamali wanatakiwa kutengeneza vikundi vitakavyowasaidia
kuweza kupata mikopo ili waweze kujiinua kiuchumi na kuinua kipato cha mtu
mmoja mmoja pamoja na taifa kwa ujumla
Niwaombe wajasiriamali kufanya uteuzi nipate watu kumi kwaajili ya kuwapeleka maonesho ya sabasaba nauli nitatoa mimi nataka nifanye hivi kwa ajili ya kuwapatia mafunzo yatakayosaidia kuinua na kubadilisha biashara zenu
Naye
Mkurugenzi wa Shirika la Viwanda na wanawake kiuchumi Bi. Abiba Saidi amewataka
wanawake kuchangamkia fursa na kusaidiana na waume zao katika kulea familia kwa
ajili ya kupunguza majukumu ya kutunza familia. Lakini pia amewataka
wajasiriamali kufanya kazi kwa vitendo ili kuweza kuingia katika soko la
ushindani
Naiomba Serikali kupitia ofisi yako Naibu Waziri wa kilimo Mh.Mavunde kuna bidhaa nyingi zinazalishwa na wajasiriamali wetu lakini changamoto kubwa ni ukosefu wa nembo ya ubora TBS, naomba wajasiriamali wapatiwe nembo ya tbs ili waweze kuingia katika soko la ushindani
0 Comments