SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu imeshauriwa kuchanganya lugha mbili katika ufundishaji ambazo ni lugha za kiuchumi na lugha ya Ufaulu ili taifa liweze kusonga mbele.
Akizungumza wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mbunge wa Jimbo la Pangawe Zanzibar Haji Amri Haji amesema kuwa nchi nyingi za ulaya zilizoendelea zimekuwa zikitumia lugha zao kwa sababu ya mfumo wa kibiashara na mfumo wa kiuchumi na imewafanya kukua kimafanikio.
Ninachotaka kumanisha ni kwamba kwa sisi Tanzania tunapaswa kubadilika katika ufundishaji wa lugha tunapaswa kuchanganya lugha mbili ya kiuchumi na lugha ya ufaulu ambapo katika ufaulu mtu anaweza kujifunza lugha kwa namna yoyote
Mimi binafsi nina mawazo kwamba ili nchi iweze kuendelea tunapaswa kuwa na lugha mama ya kiswahili na kama tunataka lugha ya ufaulu tungechanganya lucha zote sio kiingereza tu hata kifaransa na lugha nyunginezo
Haji.
0 Comments