MAAFISA Biashara nchini wametakiwa kujenga
urafiki wa karibu na wafanyabiashara hali itakayosaidia ukusanyaji wa mapato
kuongezeka katika mikoa na Halmashauri husika .
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Ofisi ya TAMISEMI Conrad Milinga kwenye kikao cha Kuthibitisha Mwongozo wa Wataalam wa biashara.
Mkurugunzi huyo amesema ni wakati sasa wa maafisa biashara kuwa na mahusiano mazuri kwa kuwa marafiki na wafanyabiasha ili kuikuza nchi kiuchumi.
Aidha amesema Serikali ya awamu ya sita imejipambanua kufungua nchi hivyo inaleta wawekezaji, kwahiyo ni vyema wawepo watekekezaji na watendaji. Ndio Maana ikaanzishwa idara hii ya uwekezaji viwanda na kuanzia ngazi ya mikoa ili iendane na lengo la Rais Samia Suluhu Hassan.
Kama Wizara wameona kuna changamoto hivyo Wanaandaa Mwongozo wa kuwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali wanapotaka kuanzisha biashara zao wajue wanaanzia wapi na kuishia wapi .
Sangu Deogratus Katibu Tawala Msaidizi katika sekretarieti Mkoa wa Kigoma viwanda na uwekezaji amesema muundo wa sekretarieti ya mikoa Viwanda na biashara ni sehemu ya Sekretarieti
Wanashukuru Serikali ya awamu ya sita baada ya kuunganisha majukumu ya Wizara ya uwekezaji viwanda na biashara na utendaji wa Serikali za Mitaa kwa kuanzisha idara hiyo ya viwanda biashara na uwekezaji ili kazi hizo ziweze kufanyika kwa wakati sahihi kwani zamani utekekezaji wa majukumu hayo yalikuwa magumu kufanyika.
Semdoe Manongi Nyale Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya biashara Wizara ya uwekezaji viwanda na biashara amesema wamekuwa na semina iliyowakutanisha makatibu wasaidizi na makatibu Tawala wasaidizi wa mikoa kupitisha juu ya nini wanataka kufanya katika wizara na utekekezaji wa majukumu yao.Sasa hivi Serikali yetu imekuwa ikihamasisha Mazingira Bora ya kufanya biashara na uwekezaji wizara inatengeneza mwongozo utakao rahisisha utendaji kazi katika ngazi za mikoa Halmashauri na Wilaya hivyo tumeona ni vyema tuwapitishe wenzetu na kuona wapi tumefikia juu ya Muongozo huu na vitu vyote vilivyokuwa vikwazo vinakwenda kuondolewa kupitia Wizara yetu ili watu wafanye kazi na kuongea lugha moja kuanzia wizara hadi ngazi ya chini.
0 Comments