WAZIRI
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi maalumu Dkt, Dorothy Gwajima
amezindua Kampeni ya Kitaifa ya kusimamia maadili ambayo itaanza mwezi Juni hadi
Disemba mwaka huu kwaajili ya kukabiliana na mmomonyoko wa waadili, inayobebwa na kauli mbiu isemayo Maadili yetu, Taifa letu
Mh,
Dkt Gwajima amezindua kampeni hiyo katika siku ya maadhimisho ya Siku ya
kimataifa ya Familia Duniani Jijini Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere square
ambapo madhimisho hayo kitaifa yamefanyika Jijini hapa
Amesema
wazazi na walezi watekeleze majukumu yao kikamilifu kuwalinda, kukaa chini na
kuzungumza na watoto wao ili kuhakikisha wanatatua changamoto walizonazo na kufatilia
maendeleo yao shuleni.
Thamani kwa kila mtu, watoto kuwasikiliza wazazi wema kijana kufuata elimu na maagizo ya wazazi lakini niwaombe wazazi muwasimamie watoto na kuzungumza nao ili kutatua changamoto wanazokumbana nazo. Kuna wazazi wamekuwa na ubaguzi katika malezi mtoto wa kike au kiume kupewa upendeleo zaidi
Na kuna wazazi wako bize kulinda mali zisipotee, niwaombe wazazi sote tunahitaji familia bora kuwasimamia watoto wetu na kupata muda mzuri wa kuzungumza nao ili kutatua changamoto zao
Gwaijma
Naye
Mwanasaikolojia Dkt, Chriss Mauki amewataka wazazi na walezi kusimamia majukumu
ya kila mmoja katika familia na kuhakikisha watoto wanapewa mafundisho
yatakayoleta manufaa katika jamii
Niwaombe sana wazazi kwasababu kuna wazazi wamekua na Tabia ambazo hazifai na watoto Wanacopy na kupaste kutoka kwa wazazi wanachokiona. Kwa mfano mzazi unamaliza siku tatu hujarudi nyumbani na ukirudi umelewa unadhani watoto wanajifunza nini kutoka kwa hawa wazazi
Kuna wazazi wamekua wakiwaeleza watoto mabaya ya mwenza aidha baba anamwambia mtoto mama yako hafai au mama anamwambia mtoto baba yako ana tabia mbaya unakuta mtoto anajenga chuki na wazazi
Dkt Mauki
Aidha
kiongozi wa dini Sheikh Alli ameiomba serikali kufanyia utafiti wa jando na
unyago ili kuweza kurudisha tabia njema na heshima katika jamii kama serikali
itaona elimu hiyo inafaa.
Zamani palikuwa na elimu ya jando na unyago watoto wetu walikua wakifundishwa maadili mema jinsi ya kuishi na watu vizuri ndio maana watu walikua wakiishi kwa maadili
Mh,
Dkt GWAJIMA amesema takwimu za mwaka 2021 zinaonyesha watoto waliolatiliwa ni
11,466 mwaka 2022 waliolawitiwa ni 12,168 hii yote inatokea majumbani na wazazi
wamekua wakiwaficha watuhumiwa na wengine wanaogopa kuripoti hivyo naomba sasa
wazazi kuwalinda watoto.
0 Comments