MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabiri Shekimweri ameongoza zoezi la kupita katika maeneo mbalimbali ya kuhamasisha matumizi ya mashine za kielektroniki (EFDs) kwa wafanyabiashara akiwa na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa kikodi Dodoma, kwa lengo la kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya matumizi ya mashine hizo.
Akizungumza mara baada ya kukagua baadhi ya maduka katika eneo la Meriwa lililopo jijini Dodoma Shekimweri amesema yeye kama Mwenyekiti wa kamati ya kodi Wilaya, moja kati ya maazimio ya vikao vyao ni kukumbushana kuwa nao wanao wajibu wa kupita kuhamasisha, kukagua,na kukumbusha matumizi ya mashine hizo za EFDs
Kampeni hii ni ya mwezi mzima tunataka kuona muitikio wa wananchi upoje kwasababu matumizi yake hupelekea kodi na mapato mbalimbali ya Serikali kuweza kupatikana, lakini pia tumepita kuona changamoto zao lakini tumefarijika kuona matumizi ni mazuri
Shekimweri
Naye Meneja Msaidizi wa TRA Mkoa wa Dodoma Ramadhan Sengo amesema Mamlaka imeanzisha kampeni ya TUWAJIBIKE lengo ni kuhamasisha wauzaji kutoa risiti halali na wateja kudai risiti inayoonesha kiwango halali walicholipa.
Kutokutumia mashine za EFDs ni kosa kisheria tutakapomkuta mtu hatumii adhabu lazima akutane nayo
Kwa upande wake Rajabu Kibwana mfanyabiashara katika eneo hilo la Meriwa amesema kama wananchi pia wanao wajibu wa kutumia mashine hizo bila kukumbushwa na Mamlaka husika kwakuwa faida ya utoaji kodi ndio chanzo cha ujenzi wa baadhi ya miradi ya maendeleo inayofanywa hapa nchini.
Hakuna mtu atakaye tujengea nchi zaidi ya sisi wananchi wenyewe ujenzi wa barabara shule na mambo mengine yote yanayofanywa na mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan yamefanywa kupitia kodi zetu hivyo sisi kama wananchi tunao wajibu wa kutoa kodi kwa kupitia mashine hizi za (EFDs)
Kibwana
0 Comments