WAZIRI wa Nchi, Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo ametoa siku 30
kwa Mameneja wa Kanda zote wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) kuendesha kampeni za kuondosha mifuko ya plastiki isiyoruhusiwa kisheria
inayochangia katika ongezeko la uchafuzi wa mazingira hususani maeneo ya
mijini.
Akitoa tamko la
Serikali kuhusu katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki katika mkutano wake na
waandishi wa habari leo Aprili 6, 2023 Dkt. Jafo amesisitiza kuwa Meneja yoyote
wa NEMC atayeshindwa kudhibiti matumizi ya mifuko hiyo katika eneo lake
atatakiwa kuachia ngazi na kuwaachia watendaji wenye uwezo wa kutimiza wajibu
huo.
Dkt. Jafo amesema
katika siku za hivi karibuni kumejitokeza changamoto ya matumizi ya vifungashio
vya plastiki kutumika kubebea bidhaa na matumizi ya mifuko isiyoruhusiwa
kisheria, kinyume cha Kanuni ya 6 ya Kanuni za Kupiga Marufuku Mifuko ya
Plastiki za Mwaka 2019 na hivyo kuibua changamoto ya usafi wa mazingira katika
maeneo mbalimbali ya miji.
Vifungashio hivyo, vinakosa sifa na hivyo kutokidhi matakwa yaliyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Hali hii inachangia katika ongezeko la uchafuzi wa mazingira hususani maeneo ya mijini na hali hii inaonesha ukiukwaji mkubwa wa Kanuni ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki unaofanywa na baadhi ya wazalishaji na wasambazaji
Dkt. Jafo.
Aidha Dkt. Jafo
amezitaka Sekretarieti za Mikoa, Majiji, Manispaa na Halmashauri za Wilaya zote
nchini kuendelea kudhibiti matumizi ya vifungashio visivyoruhusiwa kisheria kwa
kuzingatia kuwa utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki ni jukumu la wadau
wote.
Itakumbukuwa kuwa
tarehe 1 Juni, 2019, Serikali ilipiga Marufuku uzalishaji, uingizaji nchini, usafirishaji
nje ya nchi; usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki kutumika kama vibebeo
na vifungio katika bidhaa mbalimbali
0 Comments