WAZIRI wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa siku
45 kwa wawekezaji wa mradi wa uzalishaji kokoto katika Kijiji cha Mundemu Wilaya
ya Bahi mkoani Dodoma kudhibiti vumbi linalosambaa na kusababisha kero kwa wananchi.
Pia ametoa muda
huo kwa wawekezaji hao kuhakikisha wananchi hao wanalipwa fidia ili waweze kuondoka
na kupisha mradi huo vinginevyo utasitishwa kuendelea na shughuli zake.
Dkt. Jafo ametoa
maagizo hayo Aprili 04, 2023 wakati wa ziara ya kikazi kwa
lengo kukagua na kujionea hali halisi, kujadili hatua stahiki zinazofaa kutatua
changamoto zinazowakabili wananchi wanaozungukwa na mradi huo.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo amesema kuwa Serikali inathamini uwekezaji unaofanywa hapa
nchini lakini haitavumilia kuona wananchi wawekezaji wanakiuka sheria ya mazingira
hivyo wananchi kupata madhara.
Nimepata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakililamika kupata vumbi kutokana na shughuli inayofanyika hapa na tume iliundwa hapa na watu wa madini na kutoa maelekezo lakini hawakufuata sasa hatuwezi kuvumilia watu hawafuati sheria za nchi, maelekezo yangu ni hayo mawili vinginevyo mradi huu utafungwa.
Hivyo,
kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu milipuko ya baruti wakati wa kupasua miamba
alisema hilo liko chini ya sekta ya madini hivyo alitoa wito kwa wataalamu wa madini
kufika na kufuatilia changamoto hiyo.
Kwa upande
wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Godwin Gondwe amesema anamshukuru Waziri Jafo kwa kufika
katika eneo hilo na kusikiliza na kushughulikia changamoto hizo.
Ameahidi kuyasimamia
maelekezo aliyotoa na kuhakikisha wawekezaji hao wanatekeleza maelekezo hayo ndani
ya siku 45 ambazo Waziri Jafo ametoa ili kuhakikisha madhara ya vumbi hayawafikii
wananchi.
Hivi karibuni
Baraza la Taifa la Hifadhi naUsimamizi wa Mazingira (NEMC)- Kanda ya Kati kwa kushirikiana
na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi – Dodoma na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi
ilifanya Ukaguzi katika eneo la mradi huo.
0 Comments