📌 MWANDISHI WETU
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt.Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa
Kada za ualimu na Afya.
Hayo yameelezwa leo Aprili 12, 2023
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki wakati akitoa taarifa kwa
waandishi wa habari jijini Dodoma
Amesema Idadi ya watumishi watakaoajiriwa
katika Kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika shule za Msingi na
Sekondari.
Aidha, Waziri Kairuki ameeleza kuwa idadi ya
watumishi watakoajiliwa katika kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi
katika Hospitali za Halmashauri, Vito vya Afya na Zahanati.
Waziri Kairuki amesema waombaji wanatakiwa
kuomba ajira kuanzia leo April 12, hadi 25,2023 saa 5:59 usiku.
Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama zifuatazo awe mtanzania,awe na ukomo wa umri miaka 45 cheti Cha taaluma,cheti Cha kidato Cha sita na kitambulisho Cha NIDA.
Waziri Kairuki
Aidha amewataka waombaji kuepuka utapeli
utakaojitokeza wakati wa kuomba nafasi hizo.
0 Comments