RC SENYAMULE : SERIKALI IMEKUWA IKIFANYA MABORESHO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA MAJI

📌JASMINE SHAMWEPU

SERIKALI ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa ikifanya jitihada kubwa katika kufanya mabadiliko na maboresho makubwa katika Sekta ya Maji  ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji katika sekta ya maji ili kuendana na changamoto mpya zilizoko mbele ya wananchi  na mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayoendelea kwa sasa. 

Hayo ameyasema Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Sinyamule wakati wa ufunguzi wa Taftishi juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi yaliyoletwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma ( DUWASA)

Amesema lengo kubwa la Serikali katika kufanya mabadiliko haya na kuongeza uwekezaji katika sekta ya Maji ni kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma  hapa nchini na hivyo kuboresha maisha ya Wananchi wake na hatimaye kufikia lengo la asilimia 95 (kwa mijini) lililowekwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ifikapo mwaka 2025.

Awali mwakilishi wa  Mkurugezi mkuu wa Ewura Bw. George Kabelwa amesema  katika maombi haya Mamlaka ya Maji Dodoma imeomba kufanya marekebisho ya bei zitakazotumika kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia mwaka 2023/24 hadi 2025/26  kwa mujibu wa maombi yaliyowasilishwa EWURA, Mamlaka ya Maji Dodoma imebainisha kuwa marekebisho ya bei ya maji, yanalenga kupata fedha za kutosha kukidhi gharama halisi za uendeshaji na matengenezo kwa lengo la kuboresha huduma zitolewazo.

Aidha, Mamlaka ya Maji Dodoma imeeleza kuwa bei zinazopendekezwa zitaiwezesha mamlaka kumudu gharama zote za utoaji huduma   pamoja na mambo mengine, kuendelea kuongeza ubora wa maji, kuiwezesha mamlaka kuwa endelevu na kukidhi matarajio ya wana Dodoma.  

Kwa upande wa wakilishi wa wananchi ndugu Revina Petro Lamiula  ametoa maoni kwa kusema kuwa pamoja na bei kupandishwa ila wanaitaka mamlaka ya maji safi( DUWASA)  kuhakikisha wanaboresha huduma zao pamoja na kuboresha mgao wa utoaji wa maji jijini Dodoma.

 

 

 

 

 
 

Post a Comment

0 Comments