PROF NDALICHAKO : WATU MILIONI 2.9 HUPOTEZA MAISHA MAHALA PA KAZI.

📌RHODA SIMBA

IMEELEZWA kuwa takwimu za kidunia zilizotolewa kulingana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) mwaka 2022 zinaonesha kwamba zaidi ya watu milioni mbili na laki tisa (2.9) hupoteza maisha kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi huku wafanyakazi milioni 402 huumia wakiwa kazini na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa kipindi wanachopatiwa matibabu.

Hayo yamesemwa leo April 26 Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya usalama na afya mahala pa kazi.

Amesema kwa upande wa Tanzania jumla ya ajali na magonjwa yaliyoripotiwa katika Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kuanzia Julai 2019 hadi Juni 2021 ni ajali 4,993 na magonjwa 249, katika ajali hizo, vifo vilikuwa 217.



 


Post a Comment

0 Comments