NEEMA YA MAJI WAKAZI WILAYA YA CHAMWINO.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amezindua Mradi wa ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji safi lenye ujazo wa lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Jijini Dodoma ikiwa ni kuelekea kwenye maadhimisho ya sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mradi huo uliogharimu shilingi bilioni 1.6 badala ya 2.5 utawezesha kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 42 mpaka 87 katika Wilaya ya Chamwino.

Akizungumza leo Aprili 25, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa Mradi huo Senyamule, amesema kuwa maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa Mkoa wa Dodoma unaendelea kwa kuzindua miradi mbalimbali.

Niwapongeze watumishi na uongozi wote wa DUWASA mkiongozwa na Mhandisi Aron Joseph, kwa ubunifu huu wa kuokoa pesa nyingi za serikali kwa kubuni namna nzuri ya usimamizi wa ununuzi wa vifaa na kumkabidhi Mkandarasi ambaye ni SUMA JKT na yeye kutekeleza mradi huu kwa uaminifu mkubwa ukweli ni kwamba mmefanya kazi nzuri

Senyamule

Senyamule amesema Muungano umebaki kama kielelezo kwani ni miongoni mwa Muungano uliodumu na umekuwa na faida kubwa katika nchi hizi hasa katika sekta za Maendeleo.

Pia ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais ambapo ndio inayohusika na Muungano kwa kuendelea kuondoa kero za Muungano na kuendelea kuboresha na kuufanya kuwa imara na kuvutia mataifa mengine ambapo wanaendelea kujiuliza siri ni nini ya Muungano huo kudumu kwa miaka mingi.



 

Post a Comment

0 Comments