📌 MWANDISHI WETU
KATIBU
Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu amesema lengo na matarijio ya Mkoa ni kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa
kwa kuzingatia muda uliowekwa na viwango vya ubora unaotakiwa kwa kuzingatia thamani
ya fedha.
Gugu
ameyasema hayo leo tarehe 14/04/2023 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya
katika Wilaya ya Bahi kwa lengo la kukagua utekezaji wa miradi ya maendeleo
katika wilaya hiyo.
Gugu
amehimiza watumishi wanaosimamia miradi hiyo kuwajibika na kuhakikisha usimamizi
madhubuti wa miradi yote ya maendeleo na kutoa angalizo juu ya hatua zitakazochukuliwa
dhidi ya miradi ambayo haitakamika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya afya na elimu katika Halmashauri zetu, tusiwe moja ya vikwazo katika kusimamia ukamilifu wa miradi hii, tunayotaka kufanya yafanyike kwa wakati na hapa nisisitize kubwa zaidi kusiwe na viporo vya kutokamilika kwa miradi ya maendeleo. Sote tudhamirie kukamilisha kazi zote zilizopangwa kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha kwa kuzingatia mpango kazi
Gugu
Awali,
Katibu Tawala Bw. Gugu alipata wasaa wa kuzungumza na Watumishi wa Wilaya ya
Bahi na kuwataka kutumiza wajibu wao kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni
za Utumishi wa Umma.
Haki zinaenda sambamba na wajibu, hivyo timizeni wajibu wenu kikamilifu kila mmoja katika nafasi yakeKutokana na kukamilika kwa baadhi ya majengo katika Hospitali hiyo imewezesha kuanzishwa kwa huduma ya mionzi, huduma ya upasuaji ambapo mpaka sasa akina mama 212 wamefanyiwa upasuaji, uwepo wa huduma za X-Ray na Ultrasound na kutoa huduma kwa watoto waliozaliwa chini ya umri kamili wa mimba yaani Watoto njiti.
Bw.
Gugu katika ziara yake amekagua pia ujenzi wa Zahanati ya Nagulo, Shule ya
Msingi Bahi English Medium Pre and Primary School, Shule
ya Msingi Mpamantwa Barabarani na Shule ya Msingi Kigwe yenye wanafunzi
wenye mahitaji maalumu.
0 Comments