KLABU ZA WAPINGA RUSHWA ZASHAURIWA KUELIMISHA JAMII KUHUSU MADHARA YA RUSHWA

📌DODOMA

WAKATI vitendo vya rushwa vikionekana kurudisha nyuma maendeleo, vijana wanaohitimu kwenye klabu za wapinga rushwa wanahimizwa kuendelea kuelimisha wengine kuhusu madhara ya vitendo vya rushwa.

Haya yamesemwa Aprili 29, 2023 na Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango  ya Maendeleo Vijini, Fedha na Utawala Dkt. Vedastus Timothy kwenye mahafali ya Klabu ya  Wapinga Rushwa wa chuo hicho.
Ni wajibu wa kila mtu kupambana na vitendo vya rushwa si vya uadilifu. Ni fahari kwa chuo kuwa na klabu ya vijana ya  wapinga rushwa ambao wamejipambanua kupambana na rushwa.
Kwa upande wa Mkuu wa chuo hicho  Profesa Hozen Mayaya amesema rushwa haivumikiki, kama vijana wana kila sababu kuzuia vitendo hivyo.
Kama itafika sehemu  tukaacha na tukaenda vinginevyo hatutafika.Tusipopambana tutakuwa wasaliti si  Kwa  chuo bali watanzania wote.
Profesa Mayaya.

Naye, Afisa TAKUKURU Dodoma Faustine Malecha amesema , tamaa imesababisha baadhi ya vijana kujiingiza kwenye vitendo hivyo kusababisha kutokuwa wazalendo na nchi yao.
Vijana tuweke tamaa mbali. Tusingependa kesho ukamatwe na rushwa baada ya kumaliza chuo.Halafu unasikia amejihususha na  wizi wa mitihani .
Lengo kubwa la klabu hizi  ni kuwaanda vijana kuwa mstari mbele katika kupinga na kuzuia vitendo vya rushwa Ili  kuwa wazalendo kwa Taifa lao.


Post a Comment

0 Comments