MFUKO
Wa Fidia Kwa Wafanyakazi(WCF) wapunguza kiwango cha kodi ya
malimbikizo ya madeni ya michango ya nyuma kutoka asilimia(10%) hadi
kufikia asilimia (2%) ili kuhamasisha waajiri ambao hawajasajiliwa waweze
kujisajili na watekeleze wajibu wao wa kulipa michango kwa ajili ya kulinda
wafanyakazi wao dhidi ya majanga yatokanayo na kazi
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Wa
Fidia kwa Wafanyakazi Dkt John Mduma katika mkutano wake wa kueleza utekelezaji wa
majukumu ya mfuko huo katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita,
amesema WCF imetekeleza sera ya msamaha wa riba kwa waajiri waliochelewesha
mchango tangu mfuko ulipoanza ili kuondoa mzigo kwa waajiri ambao
hawakuweza kulipia wafanyakazi wao kwa sababu mbalimbali.
Limbikizo la riba limefutwa kwa wanachama wa mfuko huo na kuwabakizia kulipa Deni msingi tu ambalo ni principal kwenye mfuko,
Mduma.
Mbali
na hayo pia mfuko unajishughulisha kulipa fidia stahiki kwa wakati kwa
wafanyakazi wanaoumia, kuugua na kufariki kutokana na kazi, ambapo hadi kufikia
mwaka 2021/2022 umelipa fidia kwa wanufaika takribani 1600 na kiasi cha zaidi
ya shilingi bilioni 9.33 kililipwa.
Pia mfuko umeweza kuendeleza kasi ya ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati hasa vinavyosindika mazao ambapo mfuko umefufua mradi wa kiwanda cha chai cha mponde ambapo uzalishaji wake umeanza mwezi Oktoba 2022
Hata
hivyo mfuko umeimarisha ushirikiano wa kimkakati na wadau wengine kama
Mfuko wa Bima Ya Afya(NHIF) na hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Hospitali ya Benjamini Mkapa na hospitali
zingine zote za mikoa na za Rufaa nchini.
0 Comments