📌MWANDISHI WETU
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule
ameshiriki katika hafla ya ugawaji majiko Banifu 114 yanayotumia nishati safi
na Salama ya kupikia katika hafla iliyofanyika Wilaya ya Bahi Kijiji cha Zanka ambapo
wananchi wa kijiji hicho na kijjii cha Kigwe wamenufaika. Majiko hayo yametolewa
na jumuiya ya wanawake ya wakala wa Nishati Vijijini ambao ndio waandaaji wa
tukio hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo, Senyamule
amesema kuwa Matumizi ya kuni na Mkaa yamekuwa chanzo kikuu kinachotumika kwa
kupikia hususani Maeneo ya Vijijini na kupelekea kutumika kwa kiwango kikubwa
na hivyo kuleta athari katika mazingira.
Serikali itaendelea kuweka vivutio kwa wazalishaji na wasambazaji wa Teknolojia na bidhaa za nishati safi na salama ya kupikia na kuongeza wigo wa upatikanaji wa bidhaa pamoja na kutoa unafuu wa gharama ili kuwezesha watumiaji kutumia bidhaa hiyo
Mhe. Senyamule.
Naye Mkurugenzi Uendelezaji Masoko na Teknolojia
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Bi. Advera Mwijage amesema jiko linatumia
nishati mbili ambayo ni jiko la kuni na mkaa ambalo linaweza kutumika sehemu
yoyote na inamsaidia mwananchi au mama wa kitanzania kupunguza gharama ya
matumizi ya fedha na kupunguza ukataji wa miti ovyo.
Vilevile Mwenyekiti wa kijiji cha Kigwe Jeremia
E.Sobayi amesema kila mwananchi
anatakiwa kuwa balozi mzuri
katika matumizi sahihi ya majiko
hayo na kila mmoja wao awe mlinzi wa mwenzake ili isije kutokea mtu akafanyia
matumizi mengine nje ya malengo yaliyowekwa ya kutunza mazingira kwa kutokukata
miti hovyo.
0 Comments