MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viatilifu
Tanzania (TPHPA) yafanya ukaguzi wa viatilifu bandia kwa
wasambazaji,watengenezaji na watumiaji katika mikoa ya Iringa ,
Mtwara,Kilimanjaro na Morogoro ili kuzuia utoaji na uingizaji wa wa vitilifu
bandia nchini.
Akizungumza na wanahabari leo machi 1 jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hyo Prof. Joseph Nduguru wakati akieleza utekelezaji majukumu ya mamlaka ya afya ya mimea na viatilifu Tanzania amesema kuwa mamlaka hiyo imeweza kufanya ukaguzi na kutoa vibali 1324 vya shehena za viatilifu.
Amesema kuwa mamlaka hyo imeweza kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Kilimo Tanzania (TARI) ambapo imeweza kufanya nayo uchunguzi wa sampuli za udongo 1300 na kuweza kujua ni aina gani ya zao ambalo linawezwa kupandwa kwenye aina tofauti za udongo na aina ya mbolea inayoweza kutumika kwenye udongo huo.
Mamlaka imefanya ukaguzi kwa aina za sampuli zinazoingizwa na kutolewa ndani na nje ya nchi.
Nduguru
Pia mamlaka hiyo imeweza kuzalisha wadudu rafiki ambao wadudu hao kazi yao kubwa ni kula visumbufu ambavyo vinapatikana katika mimea kama vile magugu pamoja na viwavi jeshi.
Licha ya hivyo pia mamlaka imeweza kudhibiti nzige wa matunda ambao husababisha madhara kwa matunda pamoja na maua ya matunda katika wilaya mbalimbali ikiwemo muheza,handeni, pangani na shinyanga na kudhibiti ndege aina ya kwelea kwelea na kuweza kuokoa tani 1056 za mazao ambayo yangekuwa yameharibiwa na ndege hao
Hata hivyo mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uelewa mdogo juu ya matumizi sahihi ya viatilifu, kuwepo kwa wauzaji wa mbegu za mimea na viatilifu ambao siyo waaminifu na kusababisha uingiaji wa viatilifu bandia.
0 Comments