MTANDAO
wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetoa mafunzo ya siku mbili
kwa Mahakimu na Majaji kuhusu wajibu wa Mahakama katika kutunza na kulinda
uhuru wa kujieleza pamoja na haki za binadamu nchini.
Mratibu
wa Mtadao wa THRDC, Onesmo Olengurumwa akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini hapa, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa Mahakimu na Majaji nchini
alisema lengo ni kukumbushana wajibu katika kutekeleza majukumu ya kila siku.
Lengo la mafunzo haya ni kukumbushana masuala mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, kumekuwepo na mabadiliko mengi ya kisheria na masuala mbalimbali yanayohusu haki za binadamu hivyo wao kama watu ambao wanatoa haki kila siku katika Mahakama, wanapaswa kuyafahamu ili kulinda haki za binadamu na uhuru wa kujieleza
Olengurumwa
Amesema
pia mafunzo mengine ambayo yatatolewa ni masuala ya maadili kwa Mahakimu na
Majaji katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji wa haki katika maeneo yao.
Suala la maadili ni jambo la muhimu sana katika mahakama zetu nchini hivyo mafunzo haya pia yatasaidia kuwakumbusha Mahakimu na Majaji wajibu wao wa kutenda haki kwa kuzingatia maadili ya kazi zao
Olengurumwa
Amesema
utoaji wa mafunzo hayo ni sehemu ya Mtandao huo kuunga juhudi za serikali
katika kuboresha miundombinu ya utoaji haki nchini.
Tusiwe watu wa kulalamika tunapaswa kushiriki kuboresha Mahakama zetu kufanya kwa pamoja kama taifa huduma ya Mahakama ni huduma ya haki jukumu letu kusaidia kuboresha sekta hii ili kupunguza malalamiko yaliyopo kwa wananchi katika masuala ya haki jinai
Olengurumwa
Naibu
katibu mkuu wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (JMAT) Mary Kallomo, amesema
mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha utendaji wao wa kila siku katika kulinda
haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.
Tunahitaji kukumbushana masuala mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yetu na suala la maadili ni jambo la muhimu sana kwakuwa sisi ndiyo tunatoa haki katika Mahakama zetu
Hata
hivyo, amesema ipo haja kwa wadau wa masuala ya haki jinai nchini kutoa mafunzo
kwa kundi hilo kuhusu masuala ya kimtandao.
Teknolojia hivi sasa imekuwa sana hivyo kutokana na hali hiyo ipo haja Mahakimu na Majaji kupatiwa mafunzo ya masuala ya kimtandao ili wanapotoa huduma zao wasivunje haki za binadamu pamoja na uhuru wa kujieleza
Kallomo
0 Comments