SHIRIKA
la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limearatibu mpango wa Taifa wa
kuzuia na kupambana na Umwagikaji wa mafuta baharini ili kulinda
mazingira pamoja na viumbe hai vinavyopatikana baharini
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dodoma katika kueleza utekelezaji wa majukumu ya
Shirika la Uwakala wa Meli nchini Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw
Kaimu Abdi Mkeyenge amesema kuwa wameweza kukabiliana na changamoto ya
umwagikaji mafuta ambapo inahatarisha maisha ya viumbe hai waishio
baharini .
Amesema
pia shirika hilo linajihusisha na utekelezaji wa mikataba, itifaki na miongozo
inayotolewa na Shirika la Bahari duniani (IMO) kwa niaba ya nchi
inaporidhia ambapo hadi sasa imeridhia usainishwaji wa mikataba 24
inayojumuisha mikataba mikuu 6 ya lazima.
Shirika limeimarisha udhibiti wa usalama na ulinzi kwenye maeneo ya shughuli za bandari kwa kusimamia urasimishaji wa maeneo 20 ya kibandari katika mwambao wa bahari na maziwa kama vile Somanga-Lindi, Kunduchi-Dar es salaam na Kilongwe- Mafia,’’amesema.
Pia
shirika limeweza kukagua meli za nje zinazofika katika bandari
zetu ambapo kwa kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Disemba 2022 imekagua
meli za kigeni 36 na kuanzia Januari 2023 imekagua meli za kigeni 37 ambapo
shirika linategemea kukagua meli 61 hadi kufikia Juni 2023.
Licha ya hivyo pia shirika limesaidia katika ongezeko la idadi ya vyeti vya mabaharia waliokidhi masharti kutoka 6068 katika mwaka 2018/19 hadi kufikia 19575 katika mwaka 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 31
Hata
hivyo kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho lakini kuna
fursa mbalimbali katika sekta ya usafiri majini ambazo zinaweza kukuza uchumi
na kuongeza ajira kwa wananchi kama vile kuanzisha utaratibu wa kusajili meli
kwa masharti nafuu.
0 Comments