MFUKO wa SELF umejipanga kuhakikisha Asasi zenye kutoa Mikopo zinajengewa uwezo mkubwa wa kuhudumia wakulima na Wajasiriamali wenye uhitaji wa kifedha katika shughuli za kilimo na biashara
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Machi 1 Jijini Dodoma Meneja Masoko wa taasisi hiyo Linda Mshana amesema wapo katika kuwahudumia wakulima kwenye shughuli za pembejeo, uvunaji, uuzaji wa mazao ikiwa ni pamoja na shughuli za Mfumo wa stakabadhi mazao ghalani.
Hata hivyo amesema dhumuni la kuhakikisha Asasi hizo zinatoa Mikopo ni kuwawezesha wakulima kukidhi mahitaji ya kifedha ili kurahisisha upatikanaji wa vifaa vya kilimo na pembejeo kwa wakulima na wafugaji.
Bi.Linda ameongeza kuwa Mfuko wa SELF pia unatoa mikopo ya Mkopo wa Imarika, Mkopo wa Mtaji, Mkupo wa Mkulima, Mkopo wa Mshahara, Mkopo wa Kopa Ada, Mkopo wa pamoja na Mkopo wa Makazi
Huduma za Mfuko wa SELF zina lengo la kukuza na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Wananchi hususani wa vijijini, na hivyo kuwapa fursa ya kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kujiongezea kipato ili kuondokana na umaskini.
Tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa SELF mpaka kufikia Disemba 2022 jumla ya Mkopo uliotolewa ni shilingi bilioni 313 na wanufaika waliofikiwa tangu mfuko huu kuanzishwa ni watu 225,000.
Mpaka sasa Mfuko wa SELF una matawi ya Kanda ambayo yanahudumia nchi nzima (Tanzania Bara na Visiwani) ambayo yako katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Iringa, Mtwara, Tanga, Kahama, Geita na Zanzibar
Mfuko wa SELF ni Taasisi
iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango yenye jukumu la kutoa huduma za fedha
kwa wananchi wa kipato cha chini
Mfuko wa SELF
ulisajiliwa tarehe 14 Septemba 2014 chini ya Sheria ya kampuni ya mwaka 2002.
Ulianza kazi zake kama kampuni mnamo tarehe 1 Julai, 2015 ukichukua majukumu ya
Small Enterpreneurs Loan Facility (SELF) Project (1999/00 mpaka 2014/2015)
Mwaka 2018 serikali ilitoa uamuzi wa kuunganisha taasisi za UTT Micrifinance
Plc na SELF Microfinance Fund ili kukuza mtaji na kuongeza wigo wa utoaji wa
huduma za mikopo kwa wanachi.
0 Comments