KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa LAAC wameitimua Ofisi ya Rais Tamisem na kuipa muda wa wiki tatu, kuja na majibu ya uhalisia baada ya kushindwa kujibu hoja 12 .
Akiongea mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya LAAC Mh Halima Mdee amesema lengo la kikao hicho ni kujadili taarifa ya mwezi Machi mwaka Jana iliyotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ambapo baada ya Bunge kufanya uchambuzi waliwasilisha taarifa mwezi Novemba na ilisomwa Bungeni na kikao hicho ilikuwa kupata majibu ya kile Bunge limeelekeza.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema ziko hoja 12 ambazo zilitakiwa kujibiwa lakini baada ya kusikiliza hoja nne wakabaini kuwa Ofisi hiyo haikupeleka majibu ya uhalisia hali iliyowalazimu kuwarudisha ili wakajipange na kuzijibu hoja hizo kwa uhalisia na ufupi.
Hoja hizo 12 walizosikiliza ni pamoja na Usimamizi wa mikopo vikundi kwa wanawake,vijana na Watu wenye ulemavu, Upatikanaji wa ruzuku na Tija Katika uwekezaji.
Kila Halmashauri inatakiwa kutenga asilimia 10 lengo ni kusaidia makundi hayo kujikwamua kiuchumi lakini hapa kumekuwa na changamoto kwani kila Halmashauri zimekuwa zikitoa Shilingi bilioni 57 Hadi 67 kwa mwaka hizi Ni fedha nyingi sana kwa kipindi cha miaka 10
Ni ukweli kila Halmashauri zimekuwa zikitoa Fedha hizi lakini tatizo ni marejesho ambapo jumla ya Halmashauri 155 zimeshidwa kurejesha mikopo hiyo.
Kwa Upande wa Upatikanaji wa Ruzuku Mwenyekiti huyo amesema Halmashauri zote zinategemea ruzuku kutoka Serikali ili ziweze kujiendesha Pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri husika hivyo Kamati imeona kuna mapungufu kwani Baadhi ya Halmashauri zimependelewa kwa kupata zaidi huku wengine wakipata pungufu na Halmashauri tatu tu ndio kupata ruzuku kama ilivyotakiwa
Niwatake Wakurugenzi Mawaziri kukumbuka hii sio Business as Usual Kamati hii inahitaji Mabadiliko sisi tumepewa dhamana hivyo waende na baada ya hizo wiki tatu kuja na majibu mafupi ya kueleweka na uhalisia.
0 Comments