SERIKALI kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kuwawezesha wanawake kiuchumi ili kuwakwamua kutokana na changamoto zinazowakabili ikiwemo mila na desturi.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani inayofanyika machi 8 kila mwaka.
Amesema ni muhimu kuwepo na usawa kwa wanawake kutokana na hatua ambazo wanazichukua ili kuwasaidia wanawake kwa kuwawezesha ili kujikwamua kiuchumi kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo katika jamii.
Amesema kuwa changamoto hizo ni pamoja na vikwazo vya mila na desturi ambazo zinawakumba zaidi wanawake wenye umri mkubwa ,walemavu na wanawake wanaoishi vijijini.
Serikali imeamua kushirikiana na wadau ili kuwawezesha wanawake kiuchumi, teknolojia na kidigitali ili kuwanufaisha wanawake waweze kuwa na matumizi sahihi ya kimtandao
Amesema kuwa takwimu za dunia kuhusu kamisheni ya wanawake inaonesha kuwa wanawake na wasichana hawanufaiki na matumizi ya teknolojia ikiwa mwaka 2022 asilimia 67 ya wanawake wanaotumia mtandao na asilimia 69 ni wanaume ambapo ni sawa na asilimia 12 ukilinganisha na wanawake ni wachache.
Pia amesema kuna umuhimu wa kuenzi mawazo ya kijasiri yenye kuleta mabadiliko ya kuchochea teknolojia ikiwa ulimwengu wa leo wa karne ya 21 upo kwenye zama za kidigitali ambayo inachochea chachu yenye kuleta maendeleo kwa wanawake.
Hata hivyo Gwajima ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake chini ya wakuu wa mikoa wakiwa na vazi la batiki kila mtu kwa uwezo wake.
0 Comments