MKURUGENZI MKUU wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania(@temesatanzania) Lazaro Kilahala amewataka wateja wa Wakala upande wa Matengenezo na Huduma za Ufundi) Kuhakikisha wanafanya Malipo ya madeni yao kwa wakati ili kuwezesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na Temesa.
Kilahala ameyasema hayo Leo Jijini Dodoma alipokuwa akifungua kikao cha Wadau kutoka Taasisi za Umma, binafsi pamoja na wazabuni wanaotumia Huduma za Temesa.
Amesema Ucheleweshaji wa malipo hayo imekuwa ikikwamisha shughuli nyingi za Temesa kitu ambacho kinapelekea utoaji Huduma wa Wakala huo kwa Taifa kushuka.
Washitini wetu tunawaomba chondechonde, suala la kutulipa mtilie mkazo kwasababu msipotulipa ninyi, Temesa itaanguka na ikianguka sio faida kwenu, sio faida kwetu, sio faida kwa wazabuni wala nchi
Kilahala.
Kilahala amesema wakala wameamua kuunda timu ya Mabalozi ambayo lengo lake ni kutatua changamoto kwa wateja na kuwapa huduma wanayostahili ili kuondokana na changamoto mbalimbali za kazi.
Kwa upande wake Meneja wa Temesa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Greyson Maleko amesema wateja wanayo Haki ya kupata Huduma Bora kutoka Temesa na pia wana Haki kulipia Huduma za wakala kwa wakati husika.
0 Comments