TCU YATOA UFAFANUZI MABORESHO YA MFUMO NA FAIDA ZAKE KWA WADAU WA ELIMU

 ðŸ“ŒRAHMA HAJIA  

KATIBU mtendaji Tume Ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Professor Charles Kihampa ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika ngazi za kielimu tangu kuundwa kwa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania kama vile kuimarika kwa mifumo ya uthibiti ubora, ushauri na usimamizi wa elimu inayotolewa na vyuo vikuu hapa nchini.

Akizungumza na wanahabari leo Februari 22 jijini Dodoma katika hafla ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Tume ya vyuo vikuu Tanzania kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa serekali ya awamu ya sita, amesema kuwa moja kati ya shughuli zinazotekelezwa na tume hiyo ni pamoja na kuimarishwa kwa programu za elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu chuo kikuu.

Tume imeimarisha mifumo yake ya utoaji elimu kwa umma na hivyo kuweza kuwafikia wadau wengi zaidi.

Njia ambazo zimekuwa zikitumiwa na tume ili kufikisha elimu kwa umma ni pamoja na kutembelea wahitimu wa kidato cha sita waliopo kwenye mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa nchini kwa lengo la kuwaelimisha kuhusu udahili na kuandaa maonyesho ya elimu ya juu ya sayansi na teknolojia ambayo hufanyika kila mwaka

Hata hivyo kurahisisha na kuimarishwa kwa utoaji wa huduma za udahili na utambuzi wa Tuzo zinazotolewa na vyuo vikuu ambapo imeimarisha mifumo yake ya kielekroniki inayotumika katika utoaji wa hduma mbalimbali kwa wanchi na wadau wa elimu

Kutokana na maboresho hayo ya mfumo, taarifa mbalimbali zinazohusu elimu ya juu hapa nchini sasa zinapatikana kwa urahisi kwaajili ya matumizi ya taasisi mbalimbali za umma na binafsi

Tume hiyo imesaidia katika kuongeza fursa za elimu ya juu na idadi ya wanafunzi wanaosoma katika elimu ya juu na idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya ndani na nje ya nchi.

 

 

Post a Comment

0 Comments