KAIMU Mkurugenzi wa nishati huduma kwa wateja Martin Mwambene ameelezea sababu zinazopelekea umeme kukatika mara kwa mara hali inayopelekea kukwamisha baadhi ya shughuli za wananchi kushindwa kuendelea.
Akizungumza na waandishi wa habari leo amesema sababu zinazopelekea kukatika kwa umeme ni pamoja na mvua za vuli kuwa chache hali inayosababisha kushindwa kuzalisha megawati nyingi za umeme .
Amesema kutokana na changamoto hiyo wameweka mipango mikakati ambayo itaweza kuzalisha megawati nyingi tofauti na zamaniAmesema kuwa kwasasa wanazalisha megawati 1300 wakiwa na lengo la kufikia megawati 5000 mwaka 2025
Kwa sasa tunajitahidi kufikia megawati 5000 hadi kufikia mwaka 2025 tatizo la umeme litakua limeisha.
Lakini kwa sasa umeme umekua sawa kwa maana kwamba umeme hausumbui, kwa sasa tumepungukiwa megawati 70 tu na hii yote ni kutokana na kugundua sababu inayochangia kukatika umeme na kuweza kutenga shilingi bilioni 4 kwaajili ya marekebisho zaidi.
0 Comments