SERIKALI imeendelea kutekeleza kwa vitendo adhima yake ya kuongeza wigo wa fursa za masomo ya elimu ya juu kwa Watanzania katika kipindi cha miaka miwili.
Nafasi za masomo katika vyuo vya elimu ya juu katika program za shahada ya kwanza zimeongezeka kutoka 157,770 mwaka 2020/2021 hadi 172,168 mwaka 2020/2022 ongezeko hilo la nafasi 14,398 ni sawa na asilimia 9.1.
Profesa Charles Kihampa ni Katibu Mtendaji Tume ya vyuo Vikuu Tanzania ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari akielezea utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Profesa Kihampa amesema programu za masomo zimeruhusiwa kudahili wanafunzi wa shahada ya kwanza ambapo imeongezeka kutoka 686 mwaka 2020/2021 hadi 757 mwaka 2022/2023, waliodahiliwa katika shahada ya kwanza wameongezeka kutoka 87,934 mwaka 2020/2021 hadi 113,383 mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 28.9.
Idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu imeongezeka kutoka 259,266 mwaka 2020/2021 hadi mwaka 2021/2022 sawa na asilimia 14.1 na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kwa mwaka wa masomo aa 2022/2023.
Kutokana na hatua hizi zinazochukuliwa na Serikalie vyuo Vikuu vimeweza kuimarisha mifumo yake ya uthibiti ubora na uendeshaji wa mafunzo
Profesa Kihampa.
Aidha Profesa Kihampa amesema Tume ya vyuo vikuu Tanzania imeendelea kuandaa na kuratibu mafunzo kwa viongozi, wahadhiri na maofisa wa vyuo vikuu vya umma na binafsi hapa nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo katika usimamizi na uendeshaji wa Taasisi zao.
Hata hivyo Profesa Kihampa amesema kutokana na uelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya TCU na taratibu za uendeshaji wa Elimu ya chuo kikuu kumepunguza kwa kiasi kikubwa changamoto wanazokutana nazo wanafunzi na wadau wengine wa elimu ya juu katika kipindi hiki ikilinganishwa na miaka iliyopita.
0 Comments