RAIS
Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku kuu ya
Maridhiano Tanzania inayotarajiwa
kufanyika Machi 3 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete ulipo mkoani Dodoma
Hayo
yameelezwa leo Februari 15
jijini Dodoma na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo
Pinda katika hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Maridhiano itakayofanyika Machi 3
mwaka huu
Leo tumekutana hapa kwa ajili ya kuangalia hiyo siku ya maridhiano kitaifa tutaadhimisha kwa mambo yapi,mazungumzo yameshaanza kwa kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali
Pinda.
Pinda
ambaye ndiye Mlezi wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania amesema kazi kubwa wanayofanya ni
kuzuia kuvunjika kwa amani na utulivu kwa Taifa na kutatua mifarakano kwa kukaa chini na
kuyazungumza ili yaishe.
Kwa
upande wake Sheikh Alhad Mussa Salimu ameishukuru serikali ya awamu ya sita ya
Dtk.Samia wanavyozidi kuunga mkono na kuahidi kuwa wataendelea kuchapa kazi ili
watu wajua dhamira kuu ya jumuiya ya maradhiano.
Sisi kama jumuiya ya maridhiano ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba watanzania wanaishi kwa amani , upendo na umoja na kuona kila mtanzania naye ni mtu wa serekali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Naye
Katibu wa Jumuiya ya Maridhiano Taifa Israel Maasa amesema kuwa
jumuiya hiyo imeendelea kujiimarisha na kupinga suala la kupambana
na ndoa ya jinsia moja kwani ni mmomonyoko wa Maadili na inaenda kinyume
na mila na desturi zetu za kitanzania.
0 Comments