MITA ZA MAJI ZA MALIPO KABLA YAWA SULUHISHO

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MAMLAKA ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) imesema imefanikiwa kuwafungia wateja 6,752 mita za maji za malipo kabla (prepaid Water Meters) na kuwa  ndio Mamlaka inayoongoza  nchini kwa kufunga mita za maji  nyingi za malipo kabla.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi David Pallangyo,wakati akielezea utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo leo  Februari 27,2023, jijini Dodoma  amesema kuwa kufungwa kwa mita hizo imesaidia kupunguza malalamiko kutoka kwa wanachi na imesaidia pia kuondoa ule urundikaji wa madeni ya maji.

Tunajivunia kuwa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira ya kwanza nchini kuwafungia wanachi wetu pamoja na taasisi mita za malipo kabla (prepaid Water Meters) na imetusaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa wateja wetu pamoja na kupunguza ule mrundikano wa madeni sasa hivi hatuna tena migogoro na wateja wetu kwani unalipa unapata huduma.

Mhandisi Pallangyo

Pallangyo amesema kuwa kupitia mfumo huo wa Malipo kabla IRUWASA imefanikiwa kupunguza kiasi cha maji yasiyolipiwa kwa upande wa Iringa mjini kutoka wastani wa asilimia 24.6 mwaka 2020 hadi wastani wa asilimia 22.52 kwa mwezi Disemba 2022.

Pia Mhandisi Palangyo amesema kuwa idadi ya wateja waliounganishwa na majisafi imeongezeka kutoka 28,133 mwaka 2020 hadi 40,549 kwa mwezi Disemba 2022.

Pamoja na mafanikio hayo Mhandisi Pallangyo amezungumzia changamoto zinazoikabili Mamlaka hiyo kuwa ni uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji ,kutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika vyanzo hivyo kama vile kilimo,ufyatuaji wa  matofali,ufugaji,uchimbaji wa michanga pamoja na ukataji wa miti,ambavyo vimekuwa vikipelekea kupungua kwa maji katika kina cha mto Ruaha mdogo hasa katika kipindi cha kiangazi.

 

 

Post a Comment

0 Comments